Wanawake waonyesheni mabinti zenu baba zao, mnatupa wakati mgumu sana

jjs2017

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2019
Posts
2,025
Reaction score
4,276
Bila kupepesa macho, niwaambie hawa wanawake / wamama wenye tabia za kuficha watoto wao wakike baba zao mwache hiyo tabia kwani mnawaathiri sana kisaikolojia.

Hata kama hukumpenda mwanaume ulie zaa nae huyo binti yako, hakuna sababu ya kumnyima haki mwanao ya kumjua baba yake pindi atakapo hitaji, wewe kama ulikosea kutokana na ulimbukeni wenu acheni kumtesa mtoto wa kike.

Mwanaume unajikuta katika harakati za kutongoza tongoza gafla anatokea binti umemuelewa, katika kuchunguza chunguza unanijikuta unamuukiza baba yako yupo wapi anakuambia hajui, unajitahidi kumdadisi anasema mama amekataa kunionyesha na hadi na fikia hapa simjui na hata kama amekufa hajanambia chochote huku mtoto wa kike analia machozi ya huzuni kuu, mnajibebea laana nyie wamama wa hovyo sana..

Sasa binti kama huyu kakosa upendo au malezi ya baba na wewe bado hata kumjua baba yake tuu hutaki amjue unamaana gani, hata kama alimkataa akiwa mdogo au ukiwa na mimba yake sio sababu binti kafika miaka 18+ bado unakataa asimjue baba yake , hiyo laana ni kali sana ole wenu .mwache upumbavu na ulimbukeni wa kipuuzi..

Hata kama baba yake alifariki wewe mwonyeshe tuu hata kaburi lake, hata kama yupo kifungoni wewe mwonyeshe tuu na hata kama mlipotezana mwambie tuu binti ukweli sio unamtesa kiakili , mnatupa wakati mgumu sana tunapo uliza mwaswali kama haya tukikutana na mabinti wa aina hii

Nb. Sometime tunauliza tuu kujua chimbuko la binti pale tunapo dhamiria kumuoa
 
Mkuu hivi ulisikiliza ile kesi ya yule binti wa miaka 19 aliekifukia kichanga cha soku 1 sababu ya kutokumjua baba wa mtoto?
 
Wacha we!!
Umejiuliza machungu waliosababishiwa hadi kufikia hatua hiyo? Au umeamua kudeal na matokeo ya tatizo!!


Kutomwambia mtoto yake ni yupi kunaweza kuwa na athari kubwa zaidi kwake kisaikolojia

Kama baba m-bovu wewe mwambie tuu Yule ndio babako, huo ubovu mtoto atakutana nao mwenyewe na kukuelewa

Na tujue tuu haibadilishiki zipo baraka ambazo zinafuata mkondo toka kwa Mungu, zinashuka kwa baba kisha kwa mtoto. Sijasema Mali, nimesema baraka
Na baraka ni maneno๐Ÿ™
 
Athari ni kubwa sana, mbali tuu na uchungu mkali alio nao binti sometime binti anaongea mambo magumu sana ya kukata tamaa ambayo kama mwanaume unasema tuu kimoyo moyo Mungu mrehemu huyu binti ili aweze kukubaliana na mazingira aliyo nayo
 
ninaishi na binti ndugu wa mke wangu, yeye hajui kabisa babake. mamake alikufa yeye akiwa mdogo na hakumtaja mtu aliyemtia mimba, kwasababu inavyoonekana ilikuwa ni kama one night stand (kukutana na mfanyabiashara asiyemjua akalala naye yule jamaa akasema), ni kama wale watoto wa korosho wa Mtwara. mwanamke analala na mwanaume ambaye hamjui na yule mwanaume anaondoka hata hajui kama ametia mtu mimba huko nyumba. inaumiza sana naamini lakini ndio wanawake wa kizazi hiki walivyo. ndio maana hata ukisafiri sehemu ambayo hata haujawahi kufika, unaweza kutafuta mwanamke ukampata siku hiyohiyo na ukalala naye tena bila condom na kama ndo una magonjwa maana yake utamwachia na hatajua wewe ni nani na unaishi wapi na akipata mimba wengine haitoi. yule mtoto sasaivi ni form four na ni wakike, anaumia moyo sana na tumemcounsel kwamba Mungu pamoja na sisi tupo pamoja naye.
 
Ashukuru Mungu hamjui baba na yupo hai wenzake wanatupwa chooni. Mwambie apige goti amshukuru mama yake na Mungu kuwa hai
 
Na katika mazingira hayohayo unaweza kuwa unatongoza mwanao au mtoto wa nduguyo
 
Athari ni kubwa sana, mbali tuu na uchungu mkali alio nao binti sometime binti anaongea mambo magumu sana ya kukata tamaa ambayo kama mwanaume unasema tuu kimoyo moyo Mungu mrehemu huyu binti ili aweze kukubaliana na mazingira aliyo nayo

Na nyie wanaume mkihabarishwa mimba zenu msijenge mazingira ya kuwatesa wabeba mimba hadi kufikia huku pa kukataa kuwaonyesha watoto baba zao

Unakuta mtu kakataa mimba tena kwa viapo vikubwaaaa na dharau kwamba "....hiyo mimba sio yangu wala usirudie kunitajaaa, kwanza siwezi zaa na mwanamke kama wewe....." sa-mwanamke atafanyaje

Wanawake wengine wanalazimika kukataa kusema kwa kuhofia kuwaumiza watoto wao
 
Ulishalianzisha namaliza,semen mtakavyo ila jitahidini kutokukimbia mimba
 


Haya mambo sio mepesi vile
Watoto na hata Mimba nyingine hazitambulishiki muhusika ndugu
Niliwahi kutana na case moja mtoto kafika miaka20 hamjui babake kumbe babake mwenyewe ni babu yake mzaa mama

Vitu vingine laana
 
Na siku hizi mafataki walivyo na uchu kwa vitoto vidogo mtakuwa na pitia mpaka binti zenu.
 
Mtoto akisha kua mkubwa 18+ mwambie ukweli, ukweli humweka mtu huru.. kuliko kucheza na hisia za mtoto tena mtoto wa kike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ