Uko sawa kabisa wanaume wakati mwingine tunazingua sana , mbaya zaidi unakuta matunzo hamna na uwezo mtu anao.Na nyie wanaume mkihabarishwa mimba zenu msijenge mazingira ya kuwatesa wabeba mimba hadi kufikia huku pa kukataa kuwaonyesha watoto baba zao
Unakuta mtu kakataa mimba tena kwa viapo vikubwaaaa na dharau kwamba "....hiyo mimba sio yangu wala usirudie kunitajaaa, kwanza siwezi zaa na mwanamke kama wewe....." sa-mwanamke atafanyaje
Wanawake wengine wanalazimika kukataa kusema kwa kuhofia kuwaumiza watoto wao
Mdada wa watu kalea mimba mwenyewe, tena kwa masimango makubwa sana, kalea mtoto kwa tabu peke ake peke ake...leo mtoto kawa mtu...kuna jamaa anataka kuteleza tu...hamna kitu kama hicho....huo utakatifu tutaukuta mbinguni tu...
Enyi wanawake nawaambia ikitokea kuna mwanaume kakufanyia hivyo...mwambie huyo mtoto baba yake alikufa....au alipotea na hakuwahi kurudi tena au mwambie tu kabisa baba yako alinikataa akakimbia..so sijui yuko wapi...