Katika maisha ya mwanadamu kuishi hapa duniani kuna mambo mengi sana Mungu amemficha mwanadamu na kumnyima ujuzi. Kubwa sana ni kwanini ameumbwa alivyo.
Kuna wakati huwa nakaa najitathimini mimi mwenyewe na kujiuliza kwanini mimi Mungu aliniumba hivi nilivyo jibu linakija kwa mbali sana kama mwanga hafifu kabisa katika giza toronto.
Kuna walioumbwa wanene, wembamba, weusi, weupe, warefu, wafupi, wakati, wenye nguvu sana, wenye akili sana, wenye kucheka sana, waongeaji sana, wakimya sana, wakatili sana, wakarimu sana, wenye sura nzuri sana, wenye maumbo ya kuvutia sana, wenye matako makubwa sana na yakuvutia, wenye matako makubwa sana yasiyovutia, wenye ngozi laini sana na yenye mvuto, wenye ngozi ngumu sana yenye mvuto, wenye nywele ndefu sana na za kuvutia, wenye vipilipili, wanaojiamini sana na kuwafanya wengine wajiskie salama kuwa nao, wasiojiamini kabisa wanaowapa wengine wasiwasi na hofu ya kuwa nao.
Maumbile yetu tumepewa na Mungu kuweza kuishi katika mazingira tuliopo. Wazungu wamepewa ngozi nyeupe kwakua sehemu wanapoishi hakuna jua.
Waafrika wamepewa ngozi nyeusi kwa kua miale ya jua inatuchoma driectly moja kwa moja.
Ila ukiachilia mbali mazingira yetu, Mungu wetu ametuumba tulivyo tofauti tofauti kwakua ni Mungu ambaye ni Tajiri wa ubunifu Our God is Rich in Creative. Mungu ni Tajiri wa ubunifu na ndio maana kaumba kwa kila namna kwa utofauti sana.
Sio kweli Tabia ya mtu inatokana na maumbile yake la hasha bali mazingira ya malezi yake na watu aliyowazunguka. Vile vile kujiamini ni tabia mtu anayooteshewa na walezi au wazazi wake toka utoto wake.
Wapo watu wengi wanaamini maumbile fulani yataweza zaidi katika kufanya mapenzi kuliko maumbile fulani nalo sio kweli. Nimetembe kwingi nimeona mengi ufundi na umaridadi wa mtu unatokana na anavyojituma katika kile anachokifanya. Kujituma toka ndani ya nafsi mpaka nje. Wapo warefu sio wakata viuo. Wapo wafupi ni mafundi sana kitandani na kazin, wapo warefu ni magogo na wavivu kazink, wapo warefu ni moto wa kujituma haswa. Wapo wafupi wanajiamini sana na wanatoa faraja kwa wengine, wapo warefu hawajiamini kabisa na wanakatisha tamaa hata kuwa nao katima maisha. Wapo wanene ambao ni flexible wapo wembamba ambao ni visiki.
Mungu abarikiwe kwa kutuumba tofauti tofuati kwa umaridadi wake wote.
Usiringie mwili wako ringia kile kilicho ndani ya mwili wako maana ndicho haswa watu wanakihitaji kwa matumizi ya muda mrefu sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app