JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani, Mohamed Usinga ameagiza Vikundi vya Wanawake wanaliopatiwa mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, ambayo bado havijapatiwa mikopo katika Halimashauri hiyo vipewe kipaumbele kwanza ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza Mapema leo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo yamefanyika Bagamoyo Mkoani Pwani, Mwenyekiti huyo amesema kuwa kutokana na wanawake hao kujitolea kupatiwa mafunzo hayo na LHRC ambayo yataenda kuboresha na kuwasaidia katika kuendesha shughuli zao licha ya kutokuwa na Mikopo ni vema sasa wakapatiwa mikopo kama wenzao ambao tayari wanayo ili kuweza kufikia malengo yao.
Aidha amesema kuwa Katika makundi yanayopatiwa mikopo Wanawake wamekuwa waaminifu katika kuleta marejesho kwa wakati hivyo kuwa kundi ambalo si wasumbufu pindi wanavyokopa hali ambayo inayochangia kuendelea kupewa nafasi mara kwa mara ya kukopeshwa.
Pia amesema ni wakati sasa mikopo inayotolewa ikawa yenye tija ili iweze kuwainua wahusika kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wakili Anna Henga amewaasa wanawake kuhakikisha wanatafuta nafasi ya kuelewa masuala ya teknolojia na kutumia katika shughuli zao mbalimbali kwani hurahisisha mambo mbalimbali ikiwemo kuweza kuuza bidhaa zao popote pale Duniani.
Chanzo: Torchmedia