Hivi dunia hii kuna mtu anamzuia mwanamke kuwaweka kinyumba wanaume wengi kiasi kwamba wanataka wanawake waruhusiwe? Waruhusiwe na nani?? Mwanamke kama ana kifua cha kuwahimili wanaume zaidi ya mmoja, awalipie kula na kulala, awe anawatunza kwa kila kitu; atakosa wanaume wa kwenda kwake???
Hakuna mwanamke anayezuiwa kuoa wanaume kama Mswati alivyooa wanawake wengi. Ila ili afanye hivyo inabidi awe na status ya Mswati. Pale kwa Mswati wanawake hawaburuzwi kwenda, wanapanga foleni Mswati anachagua anayetaka.
Kama kuna mwanamke anaweza kuwahimili wanaume wengi kwa nini asifanye hivyo? Akipata wanaume ambao wanapenda hivyo si tatizo. Lakini akiwakosa asilalamike, Mswati akikokosa wanawake unadhani atatumia bunduki kuwaleta??
Let the women play their game, but they should know their limits!!