Mara nyingi sana napata mawazo ya watu wengi sana kuhusu uchaguzi wa mwaka huu,
nikikutana na akina mama karibia wote, wanalaumu sana JK kwa mambo alivyoyaendesha, lakini wanasema Upinzania hauwezi kushinda, eti CCM itashinda,
lakini linaloniuma sana ni kwamba wanasema kura yao hawataki kuipoteza kumpa mtu ambaye hatashinda. Najaribu kuwaelekeza kuwa hiyo ndo msg kwa kiongozi wao, lakini hawataki.
kwa hili naona kuwa watatupoteza sana maana wanataarifa juu ya utendaji mbovu wa JK lakini hawataki kumtosa kwa kura zao, Jamani tuwaelimishe popote tunapokuwa, kwa hizi siku za majeruhi!
Do not ignore the power of women ! Hawadanganyiki mwaka huu kura zao kwa Dr Slaa
Unyonge wao ndiyo unasababisha yote haya, wanapewa tuvimikopo vya laki laki huku wakitakiwa kurejesha kila wiki kwa riba iliyo juu,wanaungua na moto kutwa kwa faida ya sh alfu 3, wanatembeza bidhaa za promosheni kutwa kwa ujira wa alfu jero, Je akitokea mtu akawapa chips mayai, valuu ili wamwage radhi vizuri na spika kubwa za mzee yusuf, kanga na buku mbilimbili ndani unategemea nini?Ni kweli wanawake wamepumbazwa sana,wamepewa kanga ndani yake kuna buku 2,alafu anaambiwa katafute wenzako kumi,hawa si wengine bali ni wakina mama wa uswazi hapa tegeta,harafu kawaangalie wanavyo lazwa kwenye sakafu pale m'nyamala wakiwa wanajifungua.
WANAPENDA TABASAM LA JK SIYO SERA ZA CCM na kuwabadili ipo kazi.
Mara nyingi sana napata mawazo ya watu wengi sana kuhusu uchaguzi wa mwaka huu,
nikikutana na akina mama karibia wote, wanalaumu sana JK kwa mambo alivyoyaendesha, lakini wanasema Upinzania hauwezi kushinda, eti CCM itashinda,
lakini linaloniuma sana ni kwamba wanasema kura yao hawataki kuipoteza kumpa mtu ambaye hatashinda. Najaribu kuwaelekeza kuwa hiyo ndo msg kwa kiongozi wao, lakini hawataki.
kwa hili naona kuwa watatupoteza sana maana wanataarifa juu ya utendaji mbovu wa JK lakini hawataki kumtosa kwa kura zao, Jamani tuwaelimishe popote tunapokuwa, kwa hizi siku za majeruhi!
mimi mke wangu hapana hayumo katika ujinga huo. Anajua sukari tu imepanda toka tshs.400(2005) hadi Tshs1800(2010). Na hataki ujinga wa kanga za Tshs.500.
CHAGUA CHADEMA
Du, ndugu mimi sidhani kuwa ni sahihi, kwa sababu hii ni suala la kuangalia haki yako, maendeleo yako. Mbaya zaid ni hao wakina mama wanaoteseka na wao wanasema, sasa kwanini upate shida, au usubiri ushawishiwe ndo uchague haki yako?Wapiga kura waliowengi wanataka umewashawishi kiasi gani sio unajua kiasi gani,hivyo akina mama wakishawishika watampigia kura.
Naona lugha za mashabiki wa Chadema JF zinachukuwa sura mpya kadri uchaguzi unavyokaribia, naona wanaanza kukubali uhalisia wa matokeo ya uchaguzi ujao. Kama ni dhahiri wanawake waitaipigia kura CCM, kama ni dhahiri kwamba Chadema haijasimamisha wagombea katika majimbo kadhaa, kama ni dhahiri kwamba baadhi ya wanachama wachedema wanasikitishwa na kampeni za matusi, matumaini ya Chadema kushinda yanashikiriwa na nguzo gani? Nielimisheni.