Wanawake wawili wabadilishana waume zao ili kutafuta furaha

Wanawake wawili wabadilishana waume zao ili kutafuta furaha

Wakulonga

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
762
Reaction score
771
Wanawake wawili kutoka kaunti ya Busia, magharibi mwa Kenya wamewaacha watu na bumbuwazi mara baada ya kubadilishana waume zao kwa lengo la kutafuta furaha.

Lilian Weta mwenye umri wa 28, mama wa watoto watatu na Millicent Auma mwenye umri wa miaka 29, mwenye watoto wawili wamezua gumzo katika mtandao nchini Kenya kwa kuonekana kuwa wamefanya jambo la ajabu sana kwa wanandoa hao kuamua kubadilishana wenza.

Wiki moja iliyopita wapenzi hao waliandikishiana serikalini namna watoto watalindwa baada ya wanawake hao kubadilishana waume zao pamoja na watoto.

Wanawake hao wanadai walifikia maamuzi hayo baada ya kusukumwa na ugomvi usioisha katika familia zao.

Vyombo vya habari vya Kenya vimemripoti Lilian akisema alifikia uamuzi huo mara baada ya mume wake kumleta mwanamke mwingine katika nyumba yao ,mwezi mmoja uliopita.

"Mume wangu alinidanganya kuwa binamu yake kutoka Bungoma anakuja kututembelea hivyo niandae chakula, na sehemu ya kulala mgeni. Muda mfupi tu ulipita kuna mwanamke aliingia na kuniambia nimuachie nafasi kwa sababu hiyo ni nyumba yake sasa au anidunge kisu," Lilian alisema.

Lilian aliendelea kusimulia kuwa Auma alimwambia akamtafute mume wake na akimpata aoleke huko na kweli alimtafuta mume wa Millecent na kwenda kufunga ndoa halali wiki tatu zilizopita.

"Mwanamke huyu alikuja akilia na kulalamika kuwa mke wangu amemchukua mume wake na nyumba yake,"

"Nilimwambia kwamba kama mke wangu ndio amekufukuza kwako basi nenda ukachukue mizigo yako na watoto na uje ukae na mimi hapa," alisema Bwire ambaye alikuwa mume wa Millecent.

Ni wiki mbili sasa Lilian Weta alipoolewa na Christopher Bwire baada ya wapenzi wao kuwasaliti na wanadai kuwa hawajutii kitendo walichokifanya.

Bwire ameviambia vyombo vya habari nchini humo jinsi maisha yake yalivyobadilika na kuwa ya furaha.

"Wabaya wawili wapatane na wawili wazuri wapatane, sina msongo wa mawazo.

Siku hizi ninaamka muda ninaotaka na kulala muda ninaoaka ninakula vizuri, nina furaha sana kuwa na Lilian," alisema Bwire.

Na upande wake Lilian pia anadai kuwa ana furaha sana kukaa na Bwire.

Barasa ambaye ni mume wake Lilian zamani anasema kuwa hana haja ya kumfuata mke wake na hataki kujua chochote kumuhusu kwa sababu yeye na Auma wana furaha sana.

Chanzo: BBC
 
kwani mleta mada unataka kubadirishana mme na nani?
Sio kwamba nataka kubadilishana mume mkuu wangu, ila nimejiuliza huo uzi una madhara gani hadi waubanie. wangeuacha wazi tuone maoni ya watu. Umekosa ladha walivyoufunga ujue
 
Hivi kwanini mambo yoote ya kipumbavu yanatokea Kenya tu sio Uganda ,Rwanda au TZ ?.au ndo wanajitaidi kuwaiga wazungu mila zao . maana sasa hv nikisoma kichwa cha habari nikiona upumbavu tu bc najia hii itakua Kenya na ukiingia ndani ya habari husika utaona kweli Kenya, leo asubuhi nimeingia operamin nikaona kichwa cha habari na picha ya Mama mmoja akiwa na bango anatafuta bwana wa kumuoa kachoka kukaa bachela hahahahaha bc kabla cjafungua nikasema bc itakua Kenya na kweli hukohuko .sasa najiuliza kwani %kubwa watu wa Kenya wamekosa akili ya kufikiri kabla ya kutenda eeh! Maana sielewi hv mtu hata hawazi jamii itanichukuliaje utaona kila kukicha wanafanya vituko tu mara wameandamana kwa kushinikiza kupewa MKUYENGE kisawa sawa! Mara hivi mara vile inaonekana ndio asili yao watu wa huko wamekosa kitu kinachoitwa busara .
 
Inaitwa freedom of expression ambayo nyie hamna.
 
Inaitwa freedom of expression ambayo nyie hamna.
Mbona kukitokea mauaji, utekaji au watu kupotea huku Tanzania hizo habari huandikwa, vipi habari za vituko zisijulikane?. Ukweli ni kwamba Kenya ni nchi ya hovyo sana. Kwanini mambo ya kipuuzi yasisikike katika nchi zote za jirani isipokua Kenya?
 
Safi sana, hata wewe shemeji Msukuma akikushinda badala ya kuhangaika, katafte mshikaji aliyeoa kwa Wambulu mbadilishane walau wiki moja.
Kule jukwaa la MMU humu JF huwa naona nyuzi zinaanzishwa na Watanzania wanavyteseka kwenye ndoa zao, hebu jaribuni kuwa wabunifu labda....hehehe
 
Wanawake wa ki Kenya ni hatari, mara wapige wanaume wao, mara wawaue na kuwatupa kwenye makaro ya choo, Kenya ni balaa zaidi ya TZ, Mimi ndio maana nimeamua niende kuoa Afghanistan
 
Back
Top Bottom