Wanawake wawili wabadilishana waume zao ili kutafuta furaha

Wanawake wawili wabadilishana waume zao ili kutafuta furaha

Wanawake wa ki Kenya ni hatari, mara wapige wanaume wao, mara wawaue na kuwatupa kwenye makaro ya choo, Kenya ni balaa zaidi ya TZ, Mimi ndio maana nimeamua niende kuoa Afghanistan

Afghanistan utaolewa, huko huwa hawatanii na hawakawii kujilipua.
Wanawake wetu wa Kenya tunawaoa sisi, wala usithubutu maana mlivyo waoga waoga na wapole kimaisha hamtaendana, mwanamke Mkenya ili muendane lazima uwe mtu wa kujituma, mwenye bidii na kujiongeza kimaarifa, sio legelege kutwa kujilaza kwenye kochi ukimuagiza agiza.

Nawapenda sana hawa wanawake wetu, nimeoa mmoja na tunaendana freshi sana, yaani haitokei mkwame, ukifulia unawaza wapi utoe karo ya watoto unashangaa anatatua. Mkijadili naye mambo ya maendeleo, unakuta ameshapiga hatua mia mbili mbele huko yaani ana mawazo na ideas kibao. Ukimpa hela kidogo ya biashara, anapambana na kujiongeza, alianza kwa genge la vitunguu unashangaa keshaongeza pembeni Mpesa, nguo, vipodozi n.k.
Kuna siku nilikutana na wanawake wa Kikenya huko Bongo, yaani huja wenyewe wanaingia mikoani kusaka mazao ya mashambani na kuleta huku Nairobi, nilizungumza nao tukapiga stori aisei nilipenda sana huo ujasiri wao. Ndio Ukenya huo, kuthubutu.
Kuna mwengine kule Zanzibar, dada mdogo kiumri, Mkenya hana ndugu wala nani huko, lakini alianzisha kampuni yake ndogo tu na leo hii ametanua vilivyo, mifano ipo mingi sana.

Suala la mapishi inategemea na desturi, kwa mfano Watanzania na Wakenya ladha zetu tofauti likija kwenye msosi, nilipata tabu sana siku za kwanza kwanza Tanzania kabla kuzoea vyakula vyenu, ugali wenyewe rojorojo ilhali sisi huku lazima uwe mgumu. Niliwaona kama ambao hamjui mapishi, ila baadaye nikaja kugundua kila watu na desturi zao. Mhindi anapotia viungo vingi kwenye chakula chake, wewe utahisi kichefuchefu, ila kwao ndio dili hasa.
 
Wanawake wa ki Kenya ni hatari, mara wapige wanaume wao, mara wawaue na kuwatupa kwenye makaro ya choo, Kenya ni balaa zaidi ya TZ, Mimi ndio maana nimeamua niende kuoa Afghanistan
Huko utaoa suicide bomber.
 
Back
Top Bottom