Wanawake wawili wakimbilia polisi baada ya kutolewa mapepo kwa kuchapwa viboko

Wanawake wawili wakimbilia polisi baada ya kutolewa mapepo kwa kuchapwa viboko

Waumini wawili wanawake, Mercy Rono (38) na Mercy Cherotich (30) kwa sasa wanauguza majeraha baada ya kutandikwa viboko na mchungaji wao, aliyedai kuwatoa mapepo kwa njia hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko, tukio hilo limetokea kwenye Kanisa la Betheli katika eneo la Kapkwen, Kaunti ya Bomet nchini Kenya ambapo katika kuwatoa mapepo wachafu waumini hao, mchungaji aliwatandika viboko na kushindwa kuvumilia maumivu.

Inaelezwa baada ya uchungu wa viboko kuzidi wanawake hao walikimbia na kwenda kutoa taarifa polisi, huku mchungaji huyo na watu wengine waliohusika kutoroka na sasa wanatafutwa.
View attachment 3247576
😆😆😆😆.. huduma za kiroho zimevamiwa sana siku hizi na matapeli wa kiimani
 
Back
Top Bottom