Wanawake wenye ulemavu kuwekewa miundombinu rafiki katika vyumba vya kujifungulia

Wanawake wenye ulemavu kuwekewa miundombinu rafiki katika vyumba vya kujifungulia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali imeendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma za Afya kwa kuhakikisha kuwa Vituo vya kutolea huduma za afya vinawekewa miundombinu rafiki kwa wanawake wenye ulemavu kwa ajili ya kujifungulia.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel Bungeni, Aprili 14, 2022 alipokuwa akijibu swali la Stella Alex Ikupa (Viti Maalum) Mkoa wa Mara aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali katika uhakikisha wanawake walemavu wanakuwa na miundombinu rafiki kwa ajili ya kujifulia.

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali imeshalitambua tatizo hilo na kwa muda mrefu sasa marekebisho yamekuwa yakifanyika kwenye miundombinu isiyo rafiki kwa wanawake wenye ulemavu, tayari kwenye ramani mpya za ujenzi wa vituo vya afya, Hospitali na ununuzi wa vifaa tiba kwa watu wenye mahitaji maalum yamezingatiwa.

Source: Wizara ya Afya
 
Back
Top Bottom