Wanawake wenye uwezo kimaisha muoe,musingoje kuolewa.

Wanawake wenye uwezo kimaisha muoe,musingoje kuolewa.

Ndoa ilitakiwa iwe ni sehemu ya furaha na sio karaha. Na ndoa huwa hailazimishwi huwa inakuja yenyewe.Kama kweli mnapendana basi mtadumu kwenye ndoa haijalishi kitu gani....Tatizo letu siku hizi tunapenda sana kumsaidia Mungu...
Ni kweli kabisa, tena tunasaidia hata kuumba mtu tunayemtaka. mara awe mweupe, mrefu, handsome, mrembo, mwembamba nk nk nk...huku ni kuumba.
 
Ni vizuri zaidi ukawashauri wafuate misingi ya dini, kwani dini zote zinaeleza mwanaume ni nani na mwanamke amfanyie nini mwanaume katika mahusiano. Wanawake hao wenye uwezo wakielewa hilo tu mahusiano yao watayafurahia.

Misingi ya dini bali hata kanuni za kimaumbile zinataja kwamba mume ndio bosi ktk ndoa na mke awe mnyenyekevu.angalia hata viumbe wenzetu wanyama,dume anapewa heshima zote lakini kwa wadada hawa wenye uwezo na pesa zao,akunyenyekee wewe muuza machungwa?thubutuuuu!
 
Watunduru nimependa uzi wako maana umeongea ukweli mtupu. Hata mimi nathubutu kusema wanawake wengi wasomi na wenye kipato (ninaowafahamu) wako hivyo. Binafsi huwa najaribu kuongea nao, lakini shida yao kubwa niliyogundua ni kwamba wengi wao hawajielewi kama wako hivyo, halafu pia wanakopi mambo ya western women na kuyaleta Africa bila ya ku-edit.

Umeona eeh,hawajielewi,wabinafsi na hawaambiliki.utawasikia wanataka mume msomi na mwenye kipato huku wanasahau kwamba huyo msomi na mwenye kipato nae pia ana kibri chake na hawezi kubali ndoa ya malumbano ya dot com.
 
wako waume ambao kwao kuwekwa kinyumba si tatizo na chochote atafanya ili mradi awe na uhakika wa maisha,jitwalieni hao mukawalee.
 
kumbe waweza kuwa na mapesa na bado ukakosa usingizi?? nilidhani ni cc masikini tu ndio hatupati usingizi, kha pole yake! ila huwa wana maringo fulani na majivuno juu, nadhani hiyo pia huchangia!

Mie nadhani jamii ikibadili msimamo kila kitu kinawezekana maana siku zote mwanamke ambae yupo katika reproductive age akiwa na ela na elimu ya kutosha huwa katika selection ya mwanaume huwa anachagua either mtu anaelingana nae kipato au amemzidi kabisa. mie nadhani kama wakiwa hawachagui wala hawabagui kikubwa mwanaume amekidhi vigezo vingi anavyovihitaji basi wanatangaza nia, mbona wanaume wanaoa mpaka housegirl ambaye hata darasa la saba hajamaliza wakati mwanamime yupo level flani. Kinadada design hii nadhani ifike mahala wafanye talent management kwa kuibua kipaji na kukipika mpaka kikawa level flani kama kinakaka wanavyowapika wake zao kuanzia certificate mpaka anafikia degree, tatizo wengi wanataka ready made (mwanaume ambae yupo fully equipped)
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabosa, malkia mwenyewe wa uingereza aliwahi kuahirisha shughuli za kiserikali kwa sababu mume wake alikuwa anamuhitaji siku hiyo . Hii sumu ya GENDER ISSUES inayoendelea kupandikizwa vyuoni ndio inachangia hao kina dada wasiokuwa na akili kukosa waume wa kudumu nao maishani.
 
nina rafiki yangu wa kawaida tu si kimapenzi, mwanadada mjasiriamali mama wa watoto wawili na kwa sasa ni mbunge pia,ktk bunge letu tukufu.ki maumbile si haba kwani ktk kundi la warembo nae yumo.miezi miwili iliyopita alinieleza jambo ambalo kwake alidai linamkosesha raha ktk maisha na jambo lenyewe ni kukimbiwa na kila mwanaume anaempata.alidai kuna wakati huamka usiku na kulia machozi juu ya hali hiyo kwa kujihisi mwenye balaa,na kwamba ameshazunguka kwa waganga wasio na idadi bila mafanikio.nilipojaribu kumtia moyo ikawa kama nimejipalia mkaa kwani aliongeza ukaribu na mimi mara dufu na kuanza kunichukulia kama mr wake.japo sikuwahi kukutana nae kimwili niliweza kubaini mapungufu yake ktk muda huo nikajiweka pembeni mapema kabla sijamgusa mheshimiwa.kasoro moja kubwa aliyonayo ni kumfanya mwanaume kama house boy wake,yeye ni mtu wa kutoa maagizo,maelekezo na amri hali ambayo mwanaume yoyote anaejitambua hawezi kuvumilia.nimebaini kumbe hayuko peke yake,kuna wimbi kubwa la wanawake wasomi wanaomudu maisha vizuri kutokana na ajira au biashara lakini upande wa ndoa mambo si mazuri,na walio na ndoa utagundua waume zao ni wale wanaume suruali,nikakumbuka au ndio sababu hata bosi wa mjengoni nasikia hana ndoa!?kumbe huko kote mbali,hapa jf tunao kina dada wanajitokeza kutaka waume lakini ukipitia maelezo yao utagundua ndo walewale kutokana na masharti wanayoweka.hebu tujiulize inawezekanaje mwanamke ana zaidi ya miaka 30 hajaolewa na asiwe na kasoro au hila yoyote?mimi nawapa ushauri wa bure dada zangu hawa kwamba njia pekee ya kuondokana na upweke unaowakabili ni wao ndio waoe wasingoje kuolewa.wako wanaume tegezi kwa wanawake bila kujali kama wananyanyasika au la,hawa ndio suluhisho la kudumu.ni mtazamo tu,
Karibuni kuchangia

Kimsingi anatakiwa ajione kua yeye ni mwanamke wa kawaida kama wanawake wengine wenye kipato cha kawaida na pia aelewe mipaka yake kimamlaka kwa mwanaume inaishia wapi!!
 
Dah! Kumbe tunaweza kuoa? kama wanapatikana wa kuoa plz PM!
 
huyo mheshimiwa nahisi namfahamu kwa maelezo yako. kama ni yeye hujafafanua vizuri kiundani, ana tabia chafu sana kwa wanaume when it comes to relationship, tatizo hataki kukubali. mnyanyasaji kupita maelezo, uheshimiwa wake anaupeleka hadi kitandani. ataenda sana kwa waganga huyo.
 
nina rafiki yangu wa kawaida tu si kimapenzi, mwanadada mjasiriamali mama wa watoto wawili na kwa sasa ni mbunge pia,ktk bunge letu tukufu.ki maumbile si haba kwani ktk kundi la warembo nae yumo.miezi miwili iliyopita alinieleza jambo ambalo kwake alidai linamkosesha raha ktk maisha na jambo lenyewe ni kukimbiwa na kila mwanaume anaempata.alidai kuna wakati huamka usiku na kulia machozi juu ya hali hiyo kwa kujihisi mwenye balaa,na kwamba ameshazunguka kwa waganga wasio na idadi bila mafanikio.nilipojaribu kumtia moyo ikawa kama nimejipalia mkaa kwani aliongeza ukaribu na mimi mara dufu na kuanza kunichukulia kama mr wake.japo sikuwahi kukutana nae kimwili niliweza kubaini mapungufu yake ktk muda huo nikajiweka pembeni mapema kabla sijamgusa mheshimiwa.kasoro moja kubwa aliyonayo ni kumfanya mwanaume kama house boy wake,yeye ni mtu wa kutoa maagizo,maelekezo na amri hali ambayo mwanaume yoyote anaejitambua hawezi kuvumilia.nimebaini kumbe hayuko peke yake,kuna wimbi kubwa la wanawake wasomi wanaomudu maisha vizuri kutokana na ajira au biashara lakini upande wa ndoa mambo si mazuri,na walio na ndoa utagundua waume zao ni wale wanaume suruali,nikakumbuka au ndio sababu hata bosi wa mjengoni nasikia hana ndoa!?kumbe huko kote mbali,hapa jf tunao kina dada wanajitokeza kutaka waume lakini ukipitia maelezo yao utagundua ndo walewale kutokana na masharti wanayoweka.hebu tujiulize inawezekanaje mwanamke ana zaidi ya miaka 30 hajaolewa na asiwe na kasoro au hila yoyote?mimi nawapa ushauri wa bure dada zangu hawa kwamba njia pekee ya kuondokana na upweke unaowakabili ni wao ndio waoe wasingoje kuolewa.wako wanaume tegezi kwa wanawake bila kujali kama wananyanyasika au la,hawa ndio suluhisho la kudumu.ni mtazamo tu,
Karibuni kuchangia

Mimi nadhani wanapata matatizo yote haya kwa sababu wanapata wanaume walio na kipato, au elimu iliyo chini yao. Mwanamke kama huyu wala hana tatizo lolote kama atapata mwanaume ambaye anamzidi elimu na kipato.

Sasa kwa huyu rafiki yako, kwa kuwa yeye ni mbunge tu, mwambie kuanzia sasa asihangaike na wabunge wenzie au wote walio chini yake kimapato, kielimu.Ahangaike na sisi mawaziri na manaibu waziri, Raisi wastaafu na waliopo madarakani, wagombea, wafanyabiashara wakubwa.

Kama atakuwa labda ana hitaji la kungonoka tu, hapo anaweza watafuta wacheza shoo wa bendi mbali mbali hupatikana kwa urahisi.

ni hayo tu.
Naibu Waziri, Ndukidi.
 
Kumbe watu hua wanaoa kwa sababu wana uwezo kifedha na sio kwa sababu wanawapenda wale wanao waoa??umenifungua macho hapa!
 
Kwa wao wana hisia tofauti na zile za wasio na uwezo? Chezeni na hisia zao tu mbona ni kama boflo ndani ya chai? Mwanamke ukimhandle vizuri, mapenzi safi, respect na kumdekeza umemuwin hata huo uwezo atakukabidhi wewe
 
Back
Top Bottom