Wanawake wenzangu kwa hili mnanichefua sana roho yangu

Wanawake wenzangu kwa hili mnanichefua sana roho yangu

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Huwa ninakereka sana na hili suala, pia linanipa shida kujua hasa lengo la wanawake walio wengi kushupalia kufanya hivi.

Wanawake walio wengi wakubwa kwa wadogo, wanatabia ambayo mimi binafsi inaniudhi sana.
Inanishangaza sana, mwanamke mwenzangu tunakutana njiani (tukiwa tunatembea kwa miguu) wakati wa kusalimiana LAZIMA AKUANGALIE KUANZIA KWENYE UNYAYO HADI KICHWANI. Tena bila aibu anaweza kurudia hata mara mbili au zaidi anakushusha anakupandisha! Hivi wanawake wenzangu tunakaguana nini? Huwezi kusalimia mtu bila kumchambua kuanzia chini hadi juu?

Tubadilike wanawake!!!
 
In principle Wanawake huwa hampend kusalimiana barabaran tofaut na Wanaume
Huwa tunasalimiana ila kinachokera ni pale mtu anapoanza kukukagua kuanzia kidole cha mguu hadi kichwani, sasa huwa najiuliza hivi wanakagua nini?
 
Nyie wanawake bana shida sana..
Hapo wanakua wanaangalia umevaaje ili apate umbea wa kwenda kukuteta
🙄
Tuombeeni, wamama ambao wanaelekea kuwa wazee wamestaafu utumishi wa umma nao wana hii tabia!!!!
 
Ipo jamaani hata mie ninayo ila ni maalum kwa mashoga zangu au hata ndugu zangu wa karibu. Ila mie siangalii kwa ubaya jamaani. [emoji85]

Huwa namuangalia kama alivyovaa ni kachumbari basi nimwambie mmh "Mwenzangu hii gauni ungetupia na mtandio au kiatu cha aina hii ungependeza zaidi ya hapo". Hivyo tu.

Na kama kapendeza basi nitamwagia mijisifa hapo. Acha tu.
 
Wanaangalia kuthaminisha vyuma vya nani vitakuwa vimekaza zaidi kupitia mwonekano wako[emoji3]
 
Ipo jamaani hata mie ninayo ila ni maalum kwa mashoga zangu au hata ndugu zangu wa karibu. Ila mie siangalii kwa ubaya jamaani. [emoji85]

Huwa namuangalia kama alivyovaa ni kachumbari basi nimwambie mmh "Mwenzangu hii gauni ungetupia na mtandio au kiatu cha aina hii ungependeza zaidi ya hapo". Hivyo tu.

Na kama kapendeza basi nitamwagia mijisifa hapo. Acha tu.
ahahahahahh, na akiwa hajapendeza bila shaka unamwambia tu kwa nia njema. hahahaha
 
Back
Top Bottom