Huwa ninakereka sana na hili suala, pia linanipa shida kujua hasa lengo la wanawake walio wengi kushupalia kufanya hivi.
Wanawake walio wengi wakubwa kwa wadogo, wanatabia ambayo mimi binafsi inaniudhi sana.
Inanishangaza sana, mwanamke mwenzangu tunakutana njiani (tukiwa tunatembea kwa miguu) wakati wa kusalimiana LAZIMA AKUANGALIE KUANZIA KWENYE UNYAYO HADI KICHWANI. Tena bila aibu anaweza kurudia hata mara mbili au zaidi anakushusha anakupandisha! Hivi wanawake wenzangu tunakaguana nini? Huwezi kusalimia mtu bila kumchambua kuanzia chini hadi juu?
Tubadilike wanawake!!!