Sumasuma
JF-Expert Member
- Jun 23, 2011
- 342
- 110
Wanawake, watoto na mabinti visiwani Zanzibar wanadaiwa kupigwa picha za ngono za video za kuwadhalilisha ambazo husambazwa kwenye mitandao ikiwamo ya simu.
Vitendo hivyo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake vimeibuliwa na wanasheria wa Zanzibar wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika uwanja wa Bustani ya Victoria na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Akizungumzia vitendo hivyo Dk. Shein, alisema picha hizo zimevunja ndoa pia kulazimisha mwanafunzi kuhamishiwa Mombasa nchini Kenya baada ya picha za ngono zilizopigwa kusambazwa kwenye mitandao ya simu za watu mbalimbali visiwani hapa.
Rais aliitaka jamii kushirikiana na serikali kupamaba na udhalilishaji wanawake na watoto kwa sababu vitendo hivyo vinakwenda kinyume na mila na utamaduni wa Zanzibar.
Akizungumzia zaidi udhalilishaji huo Rais wa Chama cha wanasheria Zanzibar, (ZLS) Awadh Ali Said, wakati akihutubia kwenye maadhimisho hayo alisema hata watoto wa chini ya miaka 18 hupigwa picha wakati wakifanyishwa ngono na na kusambazwa mitandaoni.
Awadhi ambaye ni Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliitaka serikali kupitia upya sheria na kuweka adhabu kwa wanaotumia mitandao kudhalilisha watu wengine.
Alitaka serikali idhibiti kisheria matumizi ya mitandao ya teknolojia ya mawasiliano ili itumike kuleta maendeleo badala ya kudhalilisha watu.
Alitaka sheria za makosa ya jinai ziangaliwe upya akitaja mfano wa adhabu ya kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya ambayo ni kifungo cha miaka 20 jela na mshitakiwa kunyimwa dhamana wakati adhabu ya kumnajisi mtoto ni kifungo cha maisha lakini mshitakiwa ana haki dhamana.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alikizungumza kwenye hafla hiyo , alisema kuwapiga picha za ngono wanawake na watoto ni kinyume cha haki za binadamu na kuwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kufichua watuhumiwa.
CHANZO: NIPASHE