Wanawake Z`bar yadaiwa wanadhalilishwa

Wanawake Z`bar yadaiwa wanadhalilishwa

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
Wanawake, watoto na mabinti visiwani Zanzibar wanadaiwa kupigwa picha za ngono za video za kuwadhalilisha ambazo husambazwa kwenye mitandao ikiwamo ya simu.

Vitendo hivyo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake vimeibuliwa na wanasheria wa Zanzibar wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika uwanja wa Bustani ya Victoria na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Akizungumzia vitendo hivyo Dk. Shein, alisema picha hizo zimevunja ndoa pia kulazimisha mwanafunzi kuhamishiwa Mombasa nchini Kenya baada ya picha za ngono zilizopigwa kusambazwa kwenye mitandao ya simu za watu mbalimbali visiwani hapa.

Rais aliitaka jamii kushirikiana na serikali kupamaba na udhalilishaji wanawake na watoto kwa sababu vitendo hivyo vinakwenda kinyume na mila na utamaduni wa Zanzibar.

Akizungumzia zaidi udhalilishaji huo Rais wa Chama cha wanasheria Zanzibar, (ZLS) Awadh Ali Said, wakati akihutubia kwenye maadhimisho hayo alisema hata watoto wa chini ya miaka 18 hupigwa picha wakati wakifanyishwa ngono na na kusambazwa mitandaoni.

Awadhi ambaye ni Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliitaka serikali kupitia upya sheria na kuweka adhabu kwa wanaotumia mitandao kudhalilisha watu wengine.

Alitaka serikali idhibiti kisheria matumizi ya mitandao ya teknolojia ya mawasiliano ili itumike kuleta maendeleo badala ya kudhalilisha watu.

Alitaka sheria za makosa ya jinai ziangaliwe upya akitaja mfano wa adhabu ya kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya ambayo ni kifungo cha miaka 20 jela na mshitakiwa kunyimwa dhamana wakati adhabu ya kumnajisi mtoto ni kifungo cha maisha lakini mshitakiwa ana haki dhamana.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alikizungumza kwenye hafla hiyo , alisema kuwapiga picha za ngono wanawake na watoto ni kinyume cha haki za binadamu na kuwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kufichua watuhumiwa.

CHANZO: NIPASHE
 
si wanasema zanzibar na wazanzibari hawafanyi mambo ya najsi?, si wanachoma makanisa na maduka ya pombe, kumbe utalii wa ngono umejikita huko hadi kwa teens!?. sad to teens, shame to others
 
Au udhalilishaji huo unafanywa na watu kutoka Tanganyika?
 
ni watu gani wanaofanya vitendo hivyo, ni wabara au wenyewe?
 
Waende Mzumbe University Main campus watafute research report tittled Online Defamation and liability of ISP:critical analysis of the law in Tanzania.
 
Haya mambo nashangaa sana...usikute ni deals za wakubwa...ila kukemea kwake mara nyingi huishia majukwaani kama hivi...hakuna kitakachofanyika.....
 
Wanajidhalilisha. Hakuna mtu atakupiga picha ya utupu bila wewe mwenyewe kuridhika. Na hii siyo Zanzibar tu, ni kote.
 
Sikia ndugu yangu hivyo vitendo vimeibuka miaka hii ya karibuni na ni baada ya kuanzishwa biashara ya pombe kila eneo na kujichomoza kutoka nje ya zanzibar wasichana wanofanya biashara ya ngono hata kwenye viwanja vya mipiora.Haya yanatuharibia vijana wetu kwa vile sh500/tu zinatosha kwenda na changu dowa.Sasa ebutusaidie dawa tuondoshe uchafu huu.
si wanasema zanzibar na wazanzibari hawafanyi mambo ya najsi?, si wanachoma makanisa na maduka ya pombe, kumbe utalii wa ngono umejikita huko hadi kwa teens!?. sad to teens, shame to others
 
Sikia ndugu yangu hivyo vitendo vimeibuka miaka hii ya karibuni na ni baada ya kuanzishwa biashara ya pombe kila eneo na kujichomoza kutoka nje ya zanzibar wasichana wanofanya biashara ya ngono hata kwenye viwanja vya mipiora.Haya yanatuharibia vijana wetu kwa vile sh500/tu zinatosha kwenda na changu dowa.Sasa ebutusaidie dawa tuondoshe uchafu huu.

Una uhakika wanaofanya vitendo hivyo ni watu wasiyo wazawa wa zanzibar, na wazanzibar wote ni wasafi hawawezi kufanya hivyo?
 
Wanajidhalilisha. Hakuna mtu atakupiga picha ya utupu bila wewe mwenyewe kuridhika. Na hii siyo Zanzibar tu, ni kote.

Tena tufikiri mara mbili anapigwa picha na nani, mfanyaji mwenzie au mgeni aliyewakuta. Wengine wanafanya makusudi kutangaza biashara zao za umalaya.
 
Sikia ndugu yangu hivyo vitendo vimeibuka miaka hii ya karibuni na ni baada ya kuanzishwa biashara ya pombe kila eneo na kujichomoza kutoka nje ya zanzibar wasichana wanofanya biashara ya ngono hata kwenye viwanja vya mipiora.Haya yanatuharibia vijana wetu kwa vile sh500/tu zinatosha kwenda na changu dowa.Sasa ebutusaidie dawa tuondoshe uchafu huu.

Ukitumia mawazo haya bado tatizo litaendelea ba hatimae kuota mizizi....Hivi unawaamini sana dada zetu wazenjieeeeeeeeeee?
 
Back
Top Bottom