WANAYANGA SC MSIRUDIE KOSA HILI

octer core

Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
6
Reaction score
8
Mashabiki wa yanga walitakiwa waiombee dua na kuisapoti simba sc katika ligi ya mabingwa afrika ili kunufaika na mambo mawili katika timu yao na nchi kwa ujumla.

Jambo la kwanza, ikiwa simba itafanikiwa kufuzu robo fainali ingeifanya bodi ya mashindano ya caf kuijadili kuiongezea uwakilishi wa timu Tanzania, badala ya moja kwa ligi ya mabingwa zingekuwa mbili. Hivyo Tanzania ingekuwa inatoa wawakilishi wa tatu au zaidi pamoja na ktk shilikisho. Si lazima yanga awe mwakilishi kimataifa, hapana ila ukizungumzia uwakilishi wa timu tatu huwezi kuwaacha yanga.

Jambo la pili ambalo wanajangwani wangefaidika nalo ni kuwa, ikiwa simba sc watatinga hatua zifuatazo/ ifuatayo angeelekeza nguvu katika mashindano mawili, yaani ligi ya mabigwa na ligi. " mshika mawili moja humponyoka" usemi huo ndiyo ulikuwa umewafika vijana hawa wa msimbazi. Wangekuwa bize huku na huko jambo ambalo sina hakika kama wangeweza kulihimili. Hiyo ina maana yanga angetumia mwanya huo kupigania ligi.

Badala yake mambo yamekuwa tofauti, utawaona wanayanga aidha kwa kutokujua, makusudi au vyote kwa pamoja utawaona wawakiwa bize tena wengine wakiwa tumbo wazi kuwashangilia al ahly na As vita ili simba sc wafungwe.....wakifugwa watatolewa. Swali, je simba sc wakitupwa nje ligi ya mabingwa watabaki katika mashindo yapi ili wapate kuwakilisha nchi kimataifa? Jibu ni ligi tu, maana FA hayupo.Jenga picha Simba anashiriki ligi baada ya pote alipogusa kaambulia patupu......utaelewa tu.

Wakati mwingine msirudie tena kosa hili.
 
Yanga imekua ikishiriki michuano ya Caf kwa miaka mingi na ikiendelea kuchukua kombe la Nyumbani. Inawezekana hujui upinzani wa Yanga na Simba, Haijalishi Yanga au Simba anashiriki michuano ipi wao sikuzote ni kuombeana njaa. Kingine ambacho hujui Simba ata ikifanikiwa kupita kwenye kundi lake itaenda kucheza hatua ya Makundi ambayo kimuundo ni Robo fainaili kitu ambacho Yanga ilisha fikia mwaka 1998. Ili Simba iweze kuibeba Tanzania inatakiwa iingie nusu fainali baada ya kupenya kwenye makundi ya Robo fainali kitu ambacho hakipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikia bana...acheni kutafuta huruma.ya yanga baada ya jana kupewa penalt ya uongo msifikiri ligi mshabeba..mkikutana na marefa wanaokataa m pesa zenu mtapata tabu sana...

Bado nawaza tu hapa mbavu zina uhusiano gani na mikono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga watusapoti kwa lipi kwa sasa?kujaza uwanja?KUFA na KUPOJA ilifurika,YES we CAN ilitema,kuanzia kwa Mchina mpaka kibanda umiza. Tunajitosheleza.
 
Hakuna kitu unachosema makundi ya robo fainali,robo fainali ni knock out stage nyumbani na ugenini mshindi wa jumla mechi zote mbili vigezo na masharti kuzingatiwa anaingia nusu fainali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba.wakaze.wafanye.vizuri.na sio kutegemea dua za.yanga.. dunia nzima katika soka wapinzani hawaombeani mema. Na hiyo ndiyo raha ya mpira..everton daima hawezi kumuombea mema liverpool, vivyo hivyo kwa spurs na arsenal, liverpool na man u, barcelona.na real madrid, river plate na boca junior n.k... bila shaka.umeelewa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Duuuuh, we jamaa muongo, yanga kafika robo fainali lini... Hyo 1998 alifika hatua ya makundi yani 16 bora na sio robo fainali
 
Mimi sitaki ushabiki wenu wa utani wa jadi, lakini Kwa hilo la Penati naishangaa Azam TV kuendelea kuwaweka Ali Mayai na Salamba kama wachambuzi wakuu wa kituo. Yaani wachambuzi wanareplay tukio halafu bado wanahalalisha penati isiyokuwepo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss Yusuf mikia kulialia hawataki kumkera
 
Duuuuh, we jamaa muongo, yanga kafika robo fainali lini... Hyo 1998 alifika hatua ya makundi yani 16 bora na sio robo fainali
Unajua lakini 16 bora imeanza lini? Isije ikawa naongea na mbumbumbu!!. Mwaka 1998 Timu zilipambana zikabaki 8 yaani Robo fainali. Yanga ilikua kundi B Ilikuwepo Manning Rangers, RajaCasablanca, Asec mimosas, Yanga. Kundi A lilikua na Dynamos, Accra heart of ok, Eagle Cement, Etoile du Sahel.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu waje na shobo kwamba wameibeba Yanga kushiriki mashindano ya CAF? No way my friend.
Ni sawa na Liverpool kabebwa kwenye mbeleko ya Man U. Hawawezi kukubali.
 

Sijui umeandika nini hapa...yaani umejaa mihemuko ya ushabiki...kasoro hii haikuanza kwa Yanga kushangilia wageni pale Simba inapocheza na timu ya nje kwenye mashindano...Ni upuuzi ulioanza siku nyingi au miaka mingi...Simba nao huwa wanafanya hivyo hivyo...tena basi Simba ndiyo zaidi kabisa...Timu ngeni inapocheza na Yanga kwenye michuano muhimu na pale timu ngeni inapokuwa na mpira, utwasikia Simba wakihesabu...mooooja, mbiiiili....taaaatu..na kadhalika...Ni kitendo cha upuuzi kabisa....Halafu yupo kiongozi mmoja mnazi wa Simba na ambaye ni kiongozi wa ngazi za juu mkoani Dar es Salaam...huyo ndiyo limbukeni kabisa...yaani kwenye mechi ya Simba na Yanga eti yeye anavaa sare za Simba wakati hata kama ni mnazi wa Simba alipaswa kuonesha utofauti kidogo kwani klabu zote ni za Dar es Salaam...Yaani Rais wetu JPM ana kazi kubwa kweli kweli kuhusu teuzi za baadhi ya viongozi kwani wengi wao hawana ABC za uongozi...
 
Simba haina time na Huruma za Yanga Ni kwa faida yao tu.
Kwanaza tuna mpango wa kuua tu upinzani was jadi...we misimu mitatu unaambulia sare tu...sasa huo Ni utani wa kadi au uteja was jadi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…