Mashabiki wa yanga walitakiwa waiombee dua na kuisapoti simba sc katika ligi ya mabingwa afrika ili kunufaika na mambo mawili katika timu yao na nchi kwa ujumla.
Jambo la kwanza, ikiwa simba itafanikiwa kufuzu robo fainali ingeifanya bodi ya mashindano ya caf kuijadili kuiongezea uwakilishi wa timu Tanzania, badala ya moja kwa ligi ya mabingwa zingekuwa mbili. Hivyo Tanzania ingekuwa inatoa wawakilishi wa tatu au zaidi pamoja na ktk shilikisho. Si lazima yanga awe mwakilishi kimataifa, hapana ila ukizungumzia uwakilishi wa timu tatu huwezi kuwaacha yanga.
Jambo la pili ambalo wanajangwani wangefaidika nalo ni kuwa, ikiwa simba sc watatinga hatua zifuatazo/ ifuatayo angeelekeza nguvu katika mashindano mawili, yaani ligi ya mabigwa na ligi. " mshika mawili moja humponyoka" usemi huo ndiyo ulikuwa umewafika vijana hawa wa msimbazi. Wangekuwa bize huku na huko jambo ambalo sina hakika kama wangeweza kulihimili. Hiyo ina maana yanga angetumia mwanya huo kupigania ligi.
Badala yake mambo yamekuwa tofauti, utawaona wanayanga aidha kwa kutokujua, makusudi au vyote kwa pamoja utawaona wawakiwa bize tena wengine wakiwa tumbo wazi kuwashangilia al ahly na As vita ili simba sc wafungwe.....wakifugwa watatolewa. Swali, je simba sc wakitupwa nje ligi ya mabingwa watabaki katika mashindo yapi ili wapate kuwakilisha nchi kimataifa? Jibu ni ligi tu, maana FA hayupo.Jenga picha Simba anashiriki ligi baada ya pote alipogusa kaambulia patupu......utaelewa tu.
Wakati mwingine msirudie tena kosa hili.