Wanazuoni msaada kwa huyu jamaa msumbufu.

Wanazuoni msaada kwa huyu jamaa msumbufu.

lubamba

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2015
Posts
947
Reaction score
614
Nina ndugu yangu amekuwa Ni msumbufu sana kwa Jamii.Huyu bwana ameanza muda mrefu kuwa kero toka kwa ndugu zake hadi Jamii mzima inayomzunguka hapa kjjn.
Tatizo lilianza Kama Miaka 14 hv iliyopita baada ya kulianzisha akiwa Ni mjukuu wa marehemu kugombea urithi wa shamba kati yake na watoto wa marehemu alidai yy ndo mrithi kutokana na wosia wa marehemu.Ukoo uliingilia kati na wote waliotoa ushauri kwamba yy hawezi kupewa urithi wa shamba lote huku watoto wa marehemu wapo alianza bifu nao.Swala hilo Bahati lilipelekwa mahakamani.Sasa huyu mtu kawa kero anasumbua kwa vitisho kubambika kesi na kjj kiuzima hakuna Amani kwa usumbufu .Naomba mwangaza sheria inasemaje juu ya mtu category hii ili tumwepushe na hasira za Jamii wasije kumdhuru kutokana na kusumbuliwa.
 
MJUKUU HARITHI MALI ZA BABU
Hebu fungukeni ninyi wakazi wa Babati
kwanini msiende Mahakamani ambako Sheria ipo wazi Mjukuu huwa hana chake ni mpaka akasubiri mgao wa Baba yake (yaani mtoto wa marehemu)
pia huwa kuna maandishi ya WOSIA
fuatilieni
 
shauri lipo mahakamani.issue Ni kwamba anakuwa kero kwa mwanaukoo yeyote ambaye Alitoa ushauri Kama ulivyoelekeza kwamba hana urithi.kero Ni nyingi ila Mara nyingi .Anaenda kesi nyingi za jinai ila ushahidi concrete wa kumtia hatiani unakosekana.suspicion nyingi zina nguvu kwa ushahidi wa mazingira. Mara nyingi huaribu Mali km kuchoma nyumba moto, kuua mifugo, kuharibu mazao na Mali nyingine ambapo kwa dhahiri anakuwa Yeye lakini ushahidi unakuwa finyu kumtia hatiani.Msaada tafadhari wa kisheria jinsi ya kumdhibiti kiumbe Kama huyu.
 
kwa maelezo yake anadai yeye ni mrithi kutokana na wosia wa marehemu, kama marehemu aliwacha wosia na ukathibishwa ni halali hakuna mtu anayeweza kuutengua.Inawezekana watoto wa marehemu ama walimtelekeza baba yao au kuna vitu walifanya kinyume na maagizo ya baba yao ndio maana hakuwaweka kwenye urithi.
 
Back
Top Bottom