Iyerdoy
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,755
- 1,939
Niliwahi kusikia kwamba hao Wangoni walikuwa wanakimbia vita kutoka makabila mengine hasimu ya kusini mwa Africa na walipofika hayo maeneo ambapo ndo wapo kwa sasa ; Waliwakuta wanyama pori wengi wanazagaa hovyo tu. Lakini Wangoni wale walipotulia hapo na kujikuta kutokana na ukosefu wa chakula ukizingatia wao ni wakimbizi hawakuwa na maandalizi wala akiba ya chakula na njaa kali imewabana kwa siku nyingi; waliamua kuwawinda na kuwala wanyama wengi hadi aina fulani za wanya zikatoweka kwa kufanywa kitoweo. Baadaye alipokuja Mkoloni(Mzungu) akiwafuatilia alikerwa sana na kitendo chao cha kuwaua na kuwala wanyamapori waliokuwepo eneo hilo. Kwa hasira; mzungu yule aliwakamata na kuwakusanya Wangoni wote na kuwataka watambuane ni kundi gani waliowamaliza Tembo, Simba, Punda milia, Nyati, Mamba, n.k. Baada ya zoezi hilo la kuwaweka Wangoni katika makundi kulingana na uharibifu wa kuwala wanyama wengi hadi kusababisha kutoweka kabisa aina ya wanyama husika katika maeneo hayo, Kwa msamaha na ubinadamu; Mzungu alitoa adhabu ya jumla na ili kuweka kumbukumbu basi kila kundi lilipewa adhabu ya kulirithi jina la wanyama waliowala. e.g. Waliokula hadi kuwamaliza Tembo waliitwa Tembo au Njovu. Waliokula Punda waliitwa Mapunda; waliokula nyani waliitwa Ngonyani, waliowamaliza nyati walilazimika kukubali kuitwa Mbogo,Walio wawinda na kuwala komba ilibidi wachukue jina la Komba, waliowala nyoka ilibidi wachukue jina la Nyoka au Mwanjoka/ Mwanzioka n.k. n.k. alimradi tu ili kuweka sawa kumbukumbu zisipotee.Habari manguli wa historia,
Tunaambiwa wangoni ni moja ya makabila ya mwisho kufika Tanganyika.
Walitokea Afrika kusini miaka chini ya 200 iliyopita kwa kukimbia vita na makaburu na makabila wenzao.
Ni lini na kwa nini waliamua kutumia majina ya wanyama kama Komba, Ngonyani etc
Kwa nini walikwepa majina ya kwao?
Asanteni kwa ufafanuzi