Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Nikupe utangulizi kwanza
Nguu/ngulu inamaanisha kabila husika au eneo/mamlaka ya kabila husika. Nikitoa mfano utanielewa zaidi, yaani ukimuuliza kijana wa kinguu wewe ni kabila gani atasema mimi ni mnguu/mngulu ambapo kwa kiingereza atasema tu nguu/ngulu. Kadhalika akiulizwa kwenu ni wapi atajibu nguu/ngulu akimaanisha eneo wanaloishi wanguu
Sasa twende kwenye nilichokuandalia na hii siyo stori ya kutunga wala siyo chai za vijiweni bali ni masimulizi ya mzee mwenye heshima zake. Kama yeye aliipata historia hii kutoka kwenye vyanzo vya namna hiyo basi ni yeye tena!
Wanguu ni watu waliotokea Abesenia huko maeneo ya Ethiopia. Walikimbia vurugu za jamii za Kihabash ndipo wakashuka mpaka wakatokea Tanzania ya sasa na sehemu waliyofika wakapokewa vizuri ni Kondoa. Hapo wakapokewa na warangi na walipata mke wa kirangi anayeitwa Mbeyu (maarufu mdala mbeyu).
Walitaka kuendelea na safari zao na wenyeji wakawabariki kwa moyo mmoja wakaondoka na mwanamke yule wakaelekea upande wa mashariki mpaka wakafika Kiteto sehemu inajulikana kama Kilimbogo. Wakaweka kambi hapo na walipotaka kuendelea na safari mdala mbeyu alighairi akidai amechoka anataka kurudi nyumbani kwanza kisha atajiandaa zaidi rasmi kwa safari hiyo. Mdala Mbeyu alirudi Irangi na wala hakuwafuata tena wala wao hawakumrudia tena
Kwa kufupisha stori tu ngoja nikurudishe kwenye heading yangu. Wale jamaa kwa muda wa miaka mingi waliendelea na safari zao kwa vituo vituo na hivyo vituo ndivyo vilizalisha makabila tanzu ya kinguu. Kuna sehemu walipokelewa wakaulizwa mbona mpo kama mlivyo wageni wetu je huko mtokako hamkuwa na vitu mfano mali, mifugo nk? Wakajibu "Nekinda na mali zetu nyingi mna WAZIGUHA" wakimaanisha tulikuwa na vitu vyetu na mali za kutosha lakini wamezichukua mahasimu wetu. Hapo wale wenyeji wakawa wanawaita kwa title ya WAZIGUHA kila wanapowazungumzia au wanapozungumza nao. Hapo wale wanguu waliobaki hapo waliitwa wazigua
Wengine walikwenda wakapewa eneo la kulima mabondeni na watu walipowauliza hawa wengine juu ya wenzao majibu yaliyotolewa yalisababisha wale wa mabondeni waitwe WABONDEI. Wabondei kwa tafsiri isiyo rasmi unaweza kusema ni wa-mabondeni au wa-mashambani. Kuna wengine waliulizwa juu ya wenzao kwamba mbona walikuwa wengi na sasa wachache wakajibu WASAMBARA wakimaanisha wamesambaa au wametawanyika na hiyo ikapelekea wanguu waliotawanyika wakaitwa wasambaa baada ya kukutwa huko walipoelekea
Wanguu wengine walienda sehemu wakakuta jamii za watu wanaishi milimani basi wakawa wanawaita WAKAGULU wakimaanisha wa-kilimani na ikapelekea watu hawa ambao siyo wanguu waitwe kwa title hiyo daima. Kagulu kwa tafsiri isiyo rasmi ni kimwinuko/kamwinuko au kamlima/kimlima/kilima. Gulu ni mlima au mwinuko au dari
Kuna mambo mengi nimeyaruka kwakweli lakini laiti ningeandika yote humu basi ungeona mtiririko wa hawa wanguu ulivyokwenda mpaka kabila takribani zote za tanga zinamezwa humo. Mengine nimeyaruka kwa sababu maalumu
Wanguu wanapatikana kwa wingi mipakani mwa mikoa takribani mitano yaani Pwani kiasi (Chalinze na Bagamoyo), Morogoro (Kilosa na Gairo), Manyara (Simanjiro na Kiteto), Dodoma (Mpwapwa na Kongwa) na Tanga yenyewe ambayo ndiyo inayowabeba na kuwatambulisha (Kilindi). Kwa wale wasiojua ni kwamba wanguu ni miongoni mwa makabila ya kigosi (unaposema "mgosi" kwa jamii za kitanzania unakusudia mtu wa kabila za Tanga ingawa neno hilo kinguu lina maana ya mwanaume).
Nitoe elimu zaidi kwa faida ya asiyejua ni kwamba neno mgosi maana yake na matumizi yake kwenye jamii ya kinguu ni kama vile osie kwa wasambaa, somo kwa wamakonde/wamwera, mosi kwa warangi, ero kwa wamasai, agwe kwa wagogo, nk (wenye makabila yenu mtanirekebisha)
Kwa leo acha niishie hapa lakini nikipata nafasi nitakuletea historia ya makabila mengine tena mfano WAPARE ambapo maana yake ni wapige, ilikuwaje mpaka wakaitwa wapige, nani wapigwe na ni nani alikuwa anasema wapigwe? Nitakujuza
Wabarbaig nao kama hujui basi jina la Wamang'ati limetolewa na Wamasai wakimaanisha adui. Yaani mmasai alikuwa anamkimbia mbarbaig akimuita kuwa ni adui na watu wote wakashika jina hilo hilo
Kuna vitu au tabia zimejengeka kwa watu wa makabila fulani fulani ambapo zinahusishwa moja kwa moja na matukio ya mababu na mabibi zao kulingana na historia ya huko nyuma (ingawa binafsi siafiki hilo). Mfano makabila ya warangi, wanguu, wakagulu, Wamasai, Wamang'ati nk wote hao nina historia zao ambazo zinatajwa ndicho chanzo cha tabia zao za hivi sasa
Kwenye makabila kulingana na historia ya huko nyuma kuna makabila unakuta wanatambulika kama watoto wa wengine, wakwe wa wengine, watumishi wa wengine, nk. Hili nalo alhamdulillaah linaondoka miaka ya siku hizi siyo kama zamani ambapo unakuta hata kama ni ndoa inasitishwa kabisa watu wasioane kisa tu historia ya kabila fulani la mwenza
Kuna kabila fulani dogo mno ambalo wengi hawalijui lipo Tanga pia. Kabila hilo ni WAMBUGU ambapo wao wanajificha kwenye usambaa na upare. Inawezekana umekutana nao wengi tu mihangaikoni ukawachukulia ni wapare au wasambaa. Unakuta mtoto wa kimbugu anaweza kipare au kisambaa vizuri tu lakini kikwao hawezi. Machinga wengi kutoka Tanga ni Wambugu, biashara zao ni vyombo sana sana jamaa ni wapambanaji hasa
Hivi vikabila vidogo vidogo mara nyingi utakuta vina historia au tabia za kufanana fanana. Kuna kabila au lugha zinajulikana kama kabila/lugha za bonde la ufa nazo zinafanana tamaduni zao na ukifuatilia utakuta zote siyo za kibantu