Wankyo Nyigesa, RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Wankyo Nyigesa, RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Tunaposena JESHI LIUNDWE UPYA ndo tunamaanisha hivi, hata nidhamu naona kama imeshuka jamani!! Unawezaje kuitamani nafasi ya boss wako alieko madarakani?

Jeshi sio chama cha siasa! Huku ni sawa na kumwambia mkuu wa nchi kuwa mteule wake hatoshi!! Kwamba atafanya mazuri zaidi ya mkuu wake!!!?
 
Leo imefanyika hafla ya kumuaga aliyekuwa RPC mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa na kumkaribisha RPC Mpya wa Pwani Pius Lutumo. Wankyo Nyigesa sasa ni RPC wa mkoa wa Kagera ambae amesema anajiandaa kuwa IGP na anaamini maombi yake Amiri Jeshi mkuu ameyasikia. Amedai alijiandaa kuwa DCI na kamishna Zanzibar nafasi ambazo zimeshachukuliwa

Kuhusu IGP aliyepo sasa amesema anaamini anafanya kazi vizuri ila anaamini yeye atafanya kazi nzuri zaidi. Wankyo amemuomba Mungu akamuonyeshe Rais Samia na atakuwa amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

Binafsi naliona picha la kutisha Jeshi la Polisi, subordinate huwezi kutoka hadharani na kudai cheo cha bosi wako tena katika sehemu inayohitaji nidhamu kwenye chain of command kama polisi halafu unabaki na matajio mtendelea kufanya kazi vizuri, otherwise awe ameshapangwa na bosi wa bosi wake.

======

RPC Wankyo Nyigesa: Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ya DCI ikachukuliwa, nikajiandaa kuwa Kamishna wa Zanzibar wakachukua, sasa hivi najiandaa kuwa IGP, na ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja tafadhali niteua kuwa IGP, Mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama Mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo?,"

"Binadamu lazima uangalie mbele, natamani kuwa IGP, najua IGP aliyopo (Sirro) hajafanya makosa anafanya mazuri lakini Mimi nitafanya mazuri zaidi, matarajio yangu ni hayo, unajua Binadamu lazima uwe na malengo target ya mbele, uwe na ndoto kubwa, huwezi tu kuwa una malengo ya kwamba nitaendeela tu kuwa RPC Mimi nataka kuwa nafasi za Juu, IGP ili nifanye makubwa kwa faida ya Watanzania wengi kuliko Watanzania wa Mkoa mmoja"

"Mimi naamini siku Rais akiniota vizuri anaweza kunipa U-IGP na matamanio yangu ni kuwa IGP, na naendelea kumuomba tu Rais Samia akiona nafaa na akaomba kwa Mungu akamuonesha Mimi sio kwamba atakuwa amekosea yupo sahihi tu, amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi"

Huyo hafai katika kazi hiyo, atakuwa hovyoo.
 
Mnajaribu sana kurudisha hizo Siasa za udini udini ila kila Mkiingiza hizo 'single' studio zinakataliwa

Kikundi kinachokula Mema ya Nchi kina watu wa dini zote, makabila yote kutoka maeneo yote na kinachowaunganisha ni michongo tu…nyie mmekaa kijiweni mnahesabu majina ya kidini ya walioteuliwa

Wankyo kama ni Mktistu imekula kwake
 
Ni vyema mwanadamu kutazama mbali, tena ni nimependa zaidi aliposema apewe miaka mitatu tu then amwambie mama kazi uliyonikabidhi imetosha.

Huyu anaonekana ameshajua anachotaka kwenda kufanya, ana mipango kichwani, ameshaona mapungufu ya IGP aliyepo hivyo anataka kwenda kuyafanyia kazi.

Tatizo lililopo kwake naona litakuwa ni uhuru wa kutimiza majukumu yake, kama akiteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM lazima atasikiliza na kufuata mapendekezo yake, na hili litampunguzia nguvu ya kutimiza majukumu yake.
 
Leo imefanyika hafla ya kumuaga aliyekuwa RPC mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa na kumkaribisha RPC Mpya wa Pwani Pius Lutumo. Wankyo Nyigesa sasa ni RPC wa mkoa wa Kagera ambae amesema anajiandaa kuwa IGP na anaamini maombi yake Amiri Jeshi mkuu ameyasikia. Amedai alijiandaa kuwa DCI na kamishna Zanzibar nafasi ambazo zimeshachukuliwa

Kuhusu IGP aliyepo sasa amesema anaamini anafanya kazi vizuri ila yeye atafanya kazi nzuri zaidi. Wankyo amemuomba Mungu akamuonyeshe Rais Samia na atakuwa amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

Binafsi naliona picha la kutisha Jeshi la Polisi, subordinate huwezi kutoka hadharani na kudai cheo cha bosi wako tena katika sehemu inayohitaji nidhamu kwenye chain of command kama polisi kisha unabaki na matarajio mtendelea kufanya kazi vizuri, otherwise awe ameshapangwa na bosi wa bosi wake.

======

RPC Wankyo Nyigesa: Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ya DCI ikachukuliwa, nikajiandaa kuwa Kamishna wa Zanzibar wakachukua, sasa hivi najiandaa kuwa IGP, na ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja tafadhali niteua kuwa IGP, Mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama Mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo?,"

"Binadamu lazima uangalie mbele, natamani kuwa IGP, najua IGP aliyopo (Sirro) hajafanya makosa anafanya mazuri lakini Mimi nitafanya mazuri zaidi, matarajio yangu ni hayo, unajua Binadamu lazima uwe na malengo target ya mbele, uwe na ndoto kubwa, huwezi tu kuwa una malengo ya kwamba nitaendeela tu kuwa RPC Mimi nataka kuwa nafasi za Juu, IGP ili nifanye makubwa kwa faida ya Watanzania wengi kuliko Watanzania wa Mkoa mmoja"

"Mimi naamini siku Rais akiniota vizuri anaweza kunipa U-IGP na matamanio yangu ni kuwa IGP, na naendelea kumuomba tu Rais Samia akiona nafaa na akaomba kwa Mungu akamuonesha Mimi sio kwamba atakuwa amekosea yupo sahihi tu, amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

View attachment 2166233
Ni wale wale tuu. Kwani Azori akichukukiwa wapi? Viroba vya maiti viliokotwa wapi kama sio mkoa wa Pwani??
Wankyo ni wa kanda gani??

Hii labda Sirro ndie kapendekeza jina la home boy ili walindane.. Pole sana mzee
 
Anatamani kuinuliwa kama yule askari Magereza enzi za Mwendazake, basi asuburi maombi yake yajibiwe
 
"Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ikachukuliwa, sasa najiandaa kuwa IGP, ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja niteua kuwa IGP, najua IGP aliyopo hajafanya makosa anafanya mazuri ila nitafanya mazuri zaidi"——RPC Kagera,Wankyo
Hapo ndipo tulipofika ndani ya jeshi la Polisi, ni mwendo wa kusaka vyeo kwa mgongo wa kujipendekeza kwa wanasiasa. Walianza kwa kulogana, wakahamia kwenye kufitiana na mwisho wa siku matamalizia kwa kuuana.
 
Kasema vizuri.

Kuna ubaya gani kuwa na ndoto kubwa?

Akwa mfano mimi nikisema siku moja nataka kuwa mkurugenzi wa taasisi nayofanya kazi kuna ubaya gani?

Watu mnataka kumfitinisha Wankyo na Sirro.

Nampongeza Wankyo kuwa na mawazo makubwa na ndoto kubwa ila nimhakikishie hapo alipofika panamtosha.
Hakuna ubaya ila sio busara kuongea ndoto zako kwenye mazingira kama hayo. Huyo kamanda angekua ni afisa wa cheo cha chini kisha akajiwekea hayo malengo na akayazungumza wala isingekua na tafsiri hii ambayo nimeifikiria.

Ila unapokua na cheo kikubwa kinachokaribia na nafasi unayoitamani kisha ukaizungumza hadharani hiyo ni dhahiri unatamani cheo cha boss wako kabla ya wakati au unamwona boss wako hatoshi kwenye hiyo nafasi.

Lakini pia ingekua hiyo nafasi anayoitamani ni nafasi ya kusoma na kupanda cheo isingekua na shida maana jitihada zake zingemfikisha uko ila kwavile nafasi yenyewe ni moja na ni ya kuteuliwa kuongea hadharani hiyo ndoto nikumkosea nidhamu aliyepo kwenye hiyo nafasi. Huu ni mtazamo wangu lakini.
 
Ni vyema mwanadamu kutazama mbali, tena ni nimependa zaidi aliposema apewe miaka mitatu tu then amwambie mama kazi uliyonikabidhi imetosha.

Huyu anaonekana ameshajua anachotaka kwenda kufanya, ana mipango kichwani, ameshaona mapungufu ya IGP aliyepo hivyo anataka kwenda kuyafanyia kazi.

Tatizo lililopo kwake naona litakuwa ni uhuru wa kutimiza majukumu yake, kama akiteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM lazima atasikiliza na kufuata mapendekezo yake, na hili litampunguzia nguvu ya kutimiza majukumu yake.
Wewe unaamini hizo porojo za miaka mitatu au kua na vision. Hata hivyo Uzoefu wa kiafrika unaonyesha watu wanaojipigia debe mara nyingi wakipata hiyo nafasi wanakuaga wabovu kupindukia.

Mimi naamini kwenye uwezo wa mtu. Ukiwa na uwezo au mawazo makubwa utaonekana tu. Maana unatakiwa uanze kuonyesha uwezo na mawazo yako kuanzia pale ulipo. Kisha uwezo wako ndio ukupandishe sio kujipigia debe.
 
Back
Top Bottom