Wankyo Nyigesa, RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Wankyo Nyigesa, RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Tayar
IMG-20220329-WA0009.jpg
 
Akasome magazeti sasa tamaa mbaya sana. Akiwa IGP kesho atatamani uraisi
 
Akasome magazeti sasa tamaa mbaya sana. Akiwa IGP kesho atatamani uraisi
 
I wish I could be IGP imemtokea puani, huu ni uhaini huwezi tamani kiti cha boss wako akiwa amekikalia.
 
Duuuhhh......akipelekwa Desk Kule HQ Dom atamlilia Nani? Ngoja tuone! Au jamaa alishaweka kambi Mkoa wa Pwani ? As huwezi kutoka Bandari ya DSM Na usipite Mkoa wa Pwani!!!!!!kipolisi Pwani kitovu cha ulaji!!!!!
Yametimia ,keshapelekwa Desk HQ .....na faili la uchunguzi juu.....Ila NI homeboy yataisha!
 
Ww ndio wale wale wakipata uongozi unajitutumua kama kifutu na kununa kila sasa.
Kuna maisha nje ya kazi na vyeo, ilikuwa hafla /sherehe ulitaka awe kama yuko kwenye gwaride? Acha ushamba wa kijinga maisha sio complicated hivo
Kua kwanza...Bado yanki mno
 
Leo imefanyika hafla ya kumuaga aliyekuwa RPC mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa na kumkaribisha RPC Mpya wa Pwani Pius Lutumo. Wankyo Nyigesa sasa ni RPC wa mkoa wa Kagera ambae amesema anajiandaa kuwa IGP na anaamini maombi yake Amiri Jeshi mkuu ameyasikia. Amedai alijiandaa kuwa DCI na kamishna Zanzibar nafasi ambazo zimeshachukuliwa

Kuhusu IGP aliyepo sasa amesema anaamini anafanya kazi vizuri ila yeye atafanya kazi nzuri zaidi. Wankyo amemuomba Mungu akamuonyeshe Rais Samia na atakuwa amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

Binafsi naliona picha la kutisha Jeshi la Polisi, subordinate huwezi kutoka hadharani na kudai cheo cha bosi wako tena katika sehemu inayohitaji nidhamu kwenye chain of command kama polisi kisha unabaki na matarajio mtendelea kufanya kazi vizuri, otherwise awe ameshapangwa na bosi wa bosi wake.

======

RPC Wankyo Nyigesa: Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ya DCI ikachukuliwa, nikajiandaa kuwa Kamishna wa Zanzibar wakachukua, sasa hivi najiandaa kuwa IGP, na ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja tafadhali niteua kuwa IGP, Mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama Mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo?,"

"Binadamu lazima uangalie mbele, natamani kuwa IGP, najua IGP aliyopo (Sirro) hajafanya makosa anafanya mazuri lakini Mimi nitafanya mazuri zaidi, matarajio yangu ni hayo, unajua Binadamu lazima uwe na malengo target ya mbele, uwe na ndoto kubwa, huwezi tu kuwa una malengo ya kwamba nitaendeela tu kuwa RPC Mimi nataka kuwa nafasi za Juu, IGP ili nifanye makubwa kwa faida ya Watanzania wengi kuliko Watanzania wa Mkoa mmoja"

"Mimi naamini siku Rais akiniota vizuri anaweza kunipa U-IGP na matamanio yangu ni kuwa IGP, na naendelea kumuomba tu Rais Samia akiona nafaa na akaomba kwa Mungu akamuonesha Mimi sio kwamba atakuwa amekosea yupo sahihi tu, amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

Pia soma;

Thread 'IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu Dodoma, ACP Mwampakale awa RPC Kagera' Breaking News: - IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu Dodoma, ACP Mwampakale awa RPC Kagera
View attachment 2166233
Kweli bangi sio maji ya kunywa
 
"Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ikachukuliwa, sasa najiandaa kuwa IGP, ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja niteua kuwa IGP, najua IGP aliyopo hajafanya makosa anafanya mazuri ila nitafanya mazuri zaidi"——RPC Kagera, Wankyo
Ukisikia "uchawa "ndio kama huo sasa
 
I wish I could be IGP in Magu's voice, Magufuli mwenyewe aliitamani sembuse Wankyo[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom