Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Tabora

Sijawaelewa hao mawakili wa utetezi,mbona like kama na wao wamechangia kuwapiga nyundo wateja wao?
 
Hii sheria ya kunyongwa hadi kufa, inatekelezwa kweli hapa nchini!
 
Upande wa utetezi ukiongozwa na Amos Gehese akisaidiana na Agnes Simba waliiomba Mahakama itende haki kutokana na kosa lao ili iweze kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia kama hiyo.
Sasa walitetea nini
 
Mawakili wa utetezi si ndio wale wapo upande wa mteja, sasa iweje wamepalia moto wa makaa ya mawe kwa wateja wao imekaaje hii wakulungwa
 
"Alikuwa na tamaa ya kumiriki mifugo ya marehemu"
Alikuwa na tamaa ya kuwa diwani"
Haya mambo mawili unayathibitishaje kisheria???
Laiti majizi ya EPA,escrow(,lowasa,kikwete)yangenyongwa.
 
hii report ni ya uongo mtupu, ni kweli kuna hukumu ya hiyo kesi watu ni wanne
wawili walihukumiwa kunyongwa na wawili hukumu ya miaka miwili jela, na siyo wote wanne kunyongwa
 
Upande wa utetezi ukiongozwa na Amos Gehese akisaidiana na Agnes Simba waliiomba Mahakama itende haki kutokana na kosa lao ili iweze kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia kama hiyo
Wakali wa utetezi kawatosa mazima wateja wake
 
Sasa hao wakili wa utetezi ndio wametetea nini hapo? Halafu ushahidi gani walioutumia kuwatia hatiani?
 
Kuna watu wanafanya unyama mpaka uwetete labda ukaazime akili za masisisimiziem
Kuna watu wengi wanazani kua Mawakili wote wa utetezi hawana hofu ya Mungu hata ukikiri kua ni kweli uliuwa kwa makusudi au ulijapatia Mali kwa njia za udanganyifu bado ataendelea kukutea kua hujauwa! Kuna Mawakili wamenyooka sana na wala hawataki ujinga! Na Mawakili wa aina hiyo huwa siyo Watumwa wa pesa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…