Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Baada ya mahojiano na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi yalibainika mashimo mengine mawili na yalipofukulia ulipatikana mwili wa Gidion Samwel Mnyawi aliyekuwa Mkazi wa Makuro Mkoani Singida ambaye Nkamba Kasubi, mganga wa kienyeji alielekeza atolewe kafara kutokana na kuza shamba kwa watu waili tofauti kwa madai kwamba wakifanya hivyo fedha zitarejeshwa.
Aidha, katika shimo lingine, zilipatikana sehemu za mwili wa binadamu ambazo zilikuwa ni nyonga, mkono wa kulia na kushoto na tulieleza, kwa vile haikuweza kubaini ni mili wa nani uchunguzi zaidi ungehitajika.
Baada ya chunguzi huo na mahojiano ya kina na watuhumiwa ambao ni Selemani Shabani Nyaland @ Hango, Said Haji Msanghaa @ Mangu na Nkamba Kasubi walieleza mili huo ni wa Seleman Hussein Idd, Miaka 23, Mkazi wa Makuro Singida, ambaye walimuua kwa kumnyonga na kumfukia kwenye shimo Juni 23, 2024.
Mahojiano zaidi yalipofanyika na kwa shirikiano mkubwa wa wananchi wanaotoa taarifa za kweli na sahihi za matukio yanayotendeka dani ya jamii ya watu kupotea, Askari Polisi wataalam wa ufuatiliaji wa matukio makubwa walifanikiwa kupata taarifa kuwa, kuna muhumiwa mwingine ambaye anaitwa Miraji Shabani Nyandalu amehusika katika mauaji haya na wakafanikiwa kumkamata Agosti 25, 2024 huko katika kijiji cha Misughaa mkoani Singida akiwa anajaribu kutoroka kwa kutumia pikipiki MC 262 CYU mali ya Daudi Msanku ambaye walimuua na kumzika huko katika kijiji cha Porobanguma Wilaya ya Chemba Jijini Dodoma.
Uchunguzi uliendelea na bada ya mtuhumiwa huyu kukamatwa na kukutanishwa na watuhumiwa wenzake, ndipo Nkamba Kasubi mganga wa kienyeji, Agosti 27, 2024 alikubali kuwaongoza askari Polisi hadi kwenye mji wake mwingine uliopo Kijiji cha Porobanguma, Tarafa ya Kwamtoro Wilaya ya Chemba na kuonyesha mashimo sita ambayo walifukia watu wengine waliowaua na kuwazika.
Soma Pia: Jeshi la Polisi limetoa taarifa tukio la kijana Samwaja aliye uwawa na kukatwa sehemu zake za siri na marafiki zake
Baada ya taratibu za ufukuwaji kufanyika ilipatikana miili ya watu wafuatao;
1. Seni Jishabi, Miaka 28, Mkazi wa Kijiji cha Porobanguma ambaye alipotea toka Machi 3, 2024 na walidai kumuua na kumzika Aprili 2024, 2. Mohamed Juma, Miaka 27, Mkazi wa Nyamikumbi A Mkoa wa Singida ambaye alipotea Mei 15, 2024 na wao wameeleza walimuua kwa kumnyonga kisha kumzika,
3. Daudi Msanku, Miaka 27, Mkazi wa Gawidu Mkoani Manyara ambaye alipotea Mei 27, 2024 na baada ya kumuua walichoma mwili wake moto kisha majivu yake kuyahifadhi kwenye doo, huyu ndiye ambaye pikipiki yake alikamatwa nayo Miraji Shabani Nyalandu akijaribu kutoroka baada ya kuona watuhumiwa wenzake wanakamatwa mfululizo
na Askari Polisi,
4. Ramadhan Yusuph, Miaka 26, Mkazi wa Kidika Mkoani Manyara, ambaye walimuua Aprili 2024, 5. Mwekwa Kasubi, Miezi 4, mtoto huyu ni wa huyo mganga wa kienyeji ambapo aliuawa Machi 2023,
6. Maka Selemani Shabani Nyalandu, Miezi 2, aliuawa Juni 2023 na ni mtoto wa muhumiwa Selemani Shabani Nyalandu @ Hango. Watoto hawa walizikwa wakiwa hai kwenye zizi la mifugo, pia watuhumiwa walikiri kumuua Ramadhani Bakari Kilesa, Miaka 80, Mkazi wa Porobanguma na kutupa mwili wake katika Pori la Akiba Swangaswanga.
Maiti yake ilipatikana Julai 25, 2024 lakini ilikuwa haijabainika kuwa aliuawa na watuhumiwa hawa hadi jana Agosti 27, 2024 walipokiri kumuua na kueleza sehemu walipomtupa ili mili wake uliwe na wanyama pori lakini kwa bahati mbaya lengo lao halikutimia.
Mili ya watu hawa wote 10 iliyopatikana Mkoani Singida ni mitatu (3) na Dodoma ni saba (7) hawa wote isipokuwa aliyetupwa kwenye Pori la Swangaswanga kwani walibadili mbinu tisa walizikwa kwa kukalishwa kwenye shimo kwa namna walivyosukumwa na Imani zao za kishirikina.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za kweli na sahihi na kuendelea kukemeana kuanzia gazi ya familia ili kuzuia na kukomesha vitendo hivi vinavyoendelea kutokea ndani ya jamii kwa siri kubwa. Kila mmoja wetu tuelimishane kwa dhati, kwa kila mmoja kwa nafasi yake katika jamii ubaya na madhara ya kuendekeza imani za kishirikina, tamaa za mali bila ya kufuata maelekezo ya Mwenyezi Mungu, sheria za nchi na miiko katika jamii, kudhulumiana, kulipiza kisasi na wivu wa mapenzi.
Uchunguzi wa molongo wa matukio haya ya Singida na Dodoma unaendela pamoja na uchunguzi wa watu wengine wanao tekeleza uhalifu kama huu na kitakachobainika Umma utafahamishwa.