GE2025 Wanu Hafidh Ameir mgombea sahihi jimbo la Makunduchi, Zanzibar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

WANU HAFIDH AMEIR MGOMBEA SAHIHI JIMBO LA MAKUNDUCHI, ZANZIBAR​

Wananchi wa Jimbo la Makunduchi lililopo Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wameonyesha kufurahishwa kumpata Mhe. Wanu Hafidh Ameir kama mgombea Ubunge wa Jimbo la Makunduchi katika kipindi hiki ambacho kuna miradi mingi inayohitaji kiongozi makini wa kusimamia maendeleo.

Wanu Hafidh Ameir aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Makunduchi ni kiongozi mzoefu na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM, UWT ikiwemo kuwa;

1. Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

2. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

3. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

4. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)

Katika kipindi cha Uwakilishi na Ubunge, Wanu Hafidh Ameir amekuwa chachu ya kuleta maendeleo ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja ambapo amegusa jamii katika sekta zote ikiwemo Kuinua Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Biashara, Michezo na kuwa kiungo mzuri wa kuwaunganisha wananchi pamoja na Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wananchi wa Makunduchi tumchague Wanu Hafidh Ameir kuwa Mbunge wetu. Pamoja, tutaweza kujenga jamii yenye nguvu, iliyojikita katika maendeleo na umoja. Tuungane na Wanu Hafidh Ameir katika safari hii ya kuleta mabadiliko chanya! Tumchague Wanu Hafidh Ameir

Kwa kumchagua Wanu Hafidh Ameir, unachagua kiongozi ambaye atasimamia maslahi yako na kuhakikisha kwamba sauti yako na sauti za wana Makunduchi zinasikika.

Wanu ni kiongozi wa jamii, ni mtu ambaye anajali na anataka kuleta mabadiliko makubwa sana ya kimandeleao katika jimbo zima la Makunduchi kwa kushirikiana kwa karibu sana na Wananchi, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Soma pia

WhatsApp Image 2025-09-03 at 14.56.57.jpeg
WhatsApp Image 2025-09-03 at 14.56.58 (2).jpeg
WhatsApp Image 2025-09-03 at 14.56.58 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-09-03 at 14.56.58.jpeg
 
Hongereni Wananchi wa Makunduuchi mumepata mgombwa shupavu na mchapakazi. Chagueni kwa chaguo lenu.
 
Bila aibu anampa mwanae ubunge, mwingine ni mkuu wa usalama na makamu wa Rais hapohapo, na Waziri Mkuu kwa pamoja (maana huyu kijana sasa anamiliki vyeo vyote kwenye nchi hii).

Kiutani utani bila aibu nchi imekuwa ya kifalme. Na watu wenye busara wapo, wazee wa nchi wapo, viongozi wapo, jeshi lipo. Labda na sisi sasa tuache kulalama tu, tuchukue hatua. Ukute na wazee nao wanasema haya yanatokea wakati vijana wapo!!! Au wenzetu (wenye uzalendo) wa vyombo vya Usalama nao wanasubiri wananchi waanze.

Huyu Mama amejua kutufikisha pahala pagumu sana. Waliomkataa hata kwa kutaka katiba ipindishwe, hawakukosea.
 
Kuna mtu nimeskia anamtaja kama VP kwenye majadiliano ya Wahuni (Plan B)
 
WANU HAFIDH AMEIR MGOMBEA SAHIHI JIMBO LA MAKUNDUCHI, ZANZIBAR​

Wananchi wa Jimbo la Makunduchi lililopo Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wameonyesha kufurahishwa kumpata Mhe. Wanu Hafidh Ameir kama mgombea Ubunge wa Jimbo la Makunduchi katika kipindi hiki ambacho kuna miradi mingi inayohitaji kiongozi makini wa kusimamia maendeleo.

Wanu Hafidh Ameir aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Makunduchi ni kiongozi mzoefu na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM, UWT ikiwemo kuwa;

1. Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

2. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

3. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

4. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)

Katika kipindi cha Uwakilishi na Ubunge, Wanu Hafidh Ameir amekuwa chachu ya kuleta maendeleo ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja ambapo amegusa jamii katika sekta zote ikiwemo Kuinua Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Biashara, Michezo na kuwa kiungo mzuri wa kuwaunganisha wananchi pamoja na Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wananchi wa Makunduchi tumchague Wanu Hafidh Ameir kuwa Mbunge wetu. Pamoja, tutaweza kujenga jamii yenye nguvu, iliyojikita katika maendeleo na umoja. Tuungane na Wanu Hafidh Ameir katika safari hii ya kuleta mabadiliko chanya! Tumchague Wanu Hafidh Ameir

Kwa kumchagua Wanu Hafidh Ameir, unachagua kiongozi ambaye atasimamia maslahi yako na kuhakikisha kwamba sauti yako na sauti za wana Makunduchi zinasikika.

Wanu ni kiongozi wa jamii, ni mtu ambaye anajali na anataka kuleta mabadiliko makubwa sana ya kimandeleao katika jimbo zima la Makunduchi kwa kushirikiana kwa karibu sana na Wananchi, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Soma pia

MEneja kampeni. Habari yako bana
 
Back
Top Bottom