WANU HAFIDH AMEIR MGOMBEA SAHIHI JIMBO LA MAKUNDUCHI, ZANZIBAR
Wananchi wa Jimbo la Makunduchi lililopo Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wameonyesha kufurahishwa kumpata Mhe. Wanu Hafidh Ameir kama mgombea Ubunge wa Jimbo la Makunduchi katika kipindi hiki ambacho kuna miradi mingi inayohitaji kiongozi makini wa kusimamia maendeleo.
Wanu Hafidh Ameir aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Makunduchi ni kiongozi mzoefu na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM, UWT ikiwemo kuwa;
1. Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
2. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
4. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)
Katika kipindi cha Uwakilishi na Ubunge, Wanu Hafidh Ameir amekuwa chachu ya kuleta maendeleo ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja ambapo amegusa jamii katika sekta zote ikiwemo Kuinua Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Biashara, Michezo na kuwa kiungo mzuri wa kuwaunganisha wananchi pamoja na Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wananchi wa Makunduchi tumchague Wanu Hafidh Ameir kuwa Mbunge wetu. Pamoja, tutaweza kujenga jamii yenye nguvu, iliyojikita katika maendeleo na umoja. Tuungane na Wanu Hafidh Ameir katika safari hii ya kuleta mabadiliko chanya! Tumchague Wanu Hafidh Ameir
Kwa kumchagua Wanu Hafidh Ameir, unachagua kiongozi ambaye atasimamia maslahi yako na kuhakikisha kwamba sauti yako na sauti za wana Makunduchi zinasikika.
Wanu ni kiongozi wa jamii, ni mtu ambaye anajali na anataka kuleta mabadiliko makubwa sana ya kimandeleao katika jimbo zima la Makunduchi kwa kushirikiana kwa karibu sana na Wananchi, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Soma pia