The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Katibu Tawala wa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw. Eliasa Mtarawanje amewasisitiza wanufaika wa mikopo ya 10% kuwa waaminifu kwenye kurejesha mikopo hiyo,
Mtarawanje amesema hayo leo Machi 16, 2025 alipokutana na vikundi 42 vilivyonufaika na mikopo ikiwa ni katika kutekeleza maono ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba halmashari zote nchini zinatenga 10% kwa ajili ya mikopo ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu
Aidha amesisitiza kuwa waliopata mikopo hiyo sio kwasababu wao ni bora sana bali wamestahili kupata kwa kipindi hiki akiwataka maafisa maendeleo wote wilayani Meatu kuhakikisha wanafika kwa wananchi kuwapa elimu juu ya namna bora ya kuomba mikopo hiyo.