Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Miongoni mwa mambo ya kustaajabisha ya awamu ya tano ni sheria mpya zilizotungwa pamoja na marekebisho ya sheria za zamani waliyoyafanya.
Kuna muda ukikaa utafakari unashindwa hata kuelewa hawa watu wanafanya haya kwa lengo la kumkomoa nani? Kuna baadhi ya sheria ni za ajabu kwelikweli hadi wao wenyewe wakalazimika kuzifanyia marekebisho tena au kabla hata ya mwaka mmoja kuisha.
Tukiigusia kwa ufupi hii sheria ya bodi ya mikopo, kwa sasa mkopo huu umefanywa kama mkopo wa biashara, kwanza marejesho yake ni 15%, kwenye ripoti za CAG mara kadhaa alieleza jinsi makato hayo yalivyo kuwa mzigo mzito kwa wafanyakazi ambao wanazigo la makato mengine mengi kwenye mishahara yao.
Pili kuna kitu kinaitwa 'value 'retention fee' ambayo ni 6% ya deni lililobakia kwa kila mwaka. 'riba' hii imeongeza mzigo mzito kwa walipaji na kuna baadhi wako hatarini kutomaliza madeni yao hadi wanastaafu.
Sasa serikali inayotunga sheria za aina hii haistahili kura yako kwakua ni wazi kuwa hawajali sheria hizo zinakuumiza kiasi gani
Kwa wale mlio sekondari na mmefikia umri wa kupiga kura, ninyi ndio kabisaa msithubutu kuwapigia hawa CCM, waulizeni dada na kaka zenu waliosoma shule binafsi ni wangapi wamepata mkopo?
CCM watataka kuwalaghai kuwa 'idadi ya wanufaika imeongezeka', huu ni upotoshaji wa maksudi kabisa, ukweli ni kwamba idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa imeongezeka sana, ndio maana idadi ya wanufaika inaonekana kama imeongezeka. Lakini ukiangalia kwa asilimia, waombaji wengi zaidi wanakosa mikopo ukilinganisha na hali ilivyokua 2015 kurudi nyuma.
Bodi inawanyima mikopo wanafunzi karibia wote waliosoma shule binafsi, pia wanakomaa kuangalia makosa madogo madogo ya ujazaji form na kuyatumia kunyima watu mikopo.
Sasa hali hii hairidhishi, na ili ibadilike ni lazima ukapige kura na kumpigia mtu sahihi, Lissu ameahidi kwa dhati kuifanyia marekebisho sheria ya bodi ya mikopo pamoja na sheria nyingine nyingi za kikandamizaji za CCM.