Katiba Iliyopo ina mapungufu mengi yasiyoweza kuvumilika zaidi.
Ni wazi kuwa anayebeza jitihada zozote za kuanzishwa tena kwa mchakato wa kupata katiba mpya kiporo uliobakia, ni kwa sababu tu ya kuwa na uelewa mdogo au ni mnufaika wa moja kwa moja wa katiba mbovu hii iliyopo.
Wanaobeza jitihada hizi wamo katika makundi haya mawili tu wala si vinginevyo.
Kwa wale wasioelewa ni jukumu letu kuwaelimisha wakapate kujua kwa nini katiba mpya ni muhimu sana kwao. Labda pia kwa nini ni muhimu zaidi sasa kuliko wakati mwingine baadaye.
Hatuna haja ya kupoteza muda na wanufaika wa mfumo. Hao wanatumia mbinu na sababu zozote zikiwamo za kijinga kuona kuwa mchakato huo hautapata kurejelewa kwa kadri iwezekanavyo.
Kwa hao ilikuwa ni muda muafaka sasa kuwasusia, zikiwamo shughuli zao, na hata "nyuzi na mabandiko yao yote." Hatuna haja ya kupoteza na muda wala kuwa na marumbano yoyote ya maneno na watu hawa kwa sasa.
Kama mbwai na wajue kabisa imeshakuwa mbwai!
Wanadhani tutasusa tu uchaguzi au hatutaweza kukabiliana nao sawia kuhakikisha katiba mpya inapatikana. Kwa mawili haya, ni wajibu wetu kuona kuwa hayawi faida kwao.
Tupambane kivyetu nao wapambane na hali zao.
Au nasema uongo ndugu zangu?