Katiba Iliyopo ina mwathiri sana mtanzania na hasa yule wa kawaida. Baadhi ya maeneo husika ni haya hapa:
-------
1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe.
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe.
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu.
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi.
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe.
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi.
7. Kuna utitiri wa vigogo wenye mapato yasiyoakisi tija, wala kuwa na ridhaa ya wananchi na wasiolipa kodi wanaopata uhalali kwenye katiba hii.
8. Kwa katiba hii polisi wanaweza mshikilia mtu kwa kumbambikizia kesi hata kwa miaka kadhaa. Mhanga akaja kuachiliwa bila ya wahusika kuwajibika kwa lolote. Hili likihalalishwa na katiba hii.
9. Nk, nk.
-----------
Mkuu,
(a) wewe hulipi kodi?
(b) Wewe hubambikiziwi kesi au hujabambikiziwa kesi hata barabarani?
(c) Kama hauko sawa na wengine mbele za sheria wewe haikupi taabu?
(d) Kama walinzi wako wakuu wa haki zako hawawajibishwi na katiba, kuona haki zako ziko salama, wewe haikuhusu?
(e) unapokuwa na viongozi waovu usio na ridhaa nao wewe haikuhusu?
(f) unapokuwa na viongozi wasio na tija wewe haikuhusu?
(g) ukiibiwa au ukadhulumiwa, wewe haikuhusu?
(h) mihimili ya utawala inapokuwa haiko huru, wewe haikuhusu?
(I) nk, nk
Wewe hunufaiki na katiba mpya ila wasiasa na wahalifu? Seriously?!
Lakini labda tuanzie hapo mkuu?
NB:
(i) hakuna anayetafuta tuzo kwenye hili.
(ii) hakuna anayekulazimisha wewe au mtu yeyote kuwa sehemu ya jitihada hizi usizoona wewe umuhimu wa kuziunga mkono au kutoziunga mkono.
(iii) Japo inafahamika pana opportunists pia ambao hupenda kukaa mkao wa mafanikio tu. Yaani upande wa mlo tu. Wao huwa ni marafiki wa Mungu na Shetani at the same time.
Aghalabu kwenye mpambano huwa neutral kuchagua upande wa ushindi baada ya vita.
Au nasema uongo ndugu zangu akina
joka kuu Yoda BAK johnthebaptist na wazalendo wenzangu?