Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Licha ya Mamlaka ya TAKUKURU Temeke kushauri utaratibu wa Daladala kufika hadi Kituo cha Buza Kanisani badala ya kuishia katika kile kituo chao kipya cha Mama Kibonge, yaani ratiba zirejee kama ilivyokuwa awali, bado mambo yamekuwa magumu kutekelezeka.
Mjadala wa awali ~ TAKUKURU: Tunafanya uchunguzi Kituo cha Buza Kanisani kuhamishwa, tunashauri kwa sasa utaratibu wa zamani urejee
Bado kumeendelea kuwa na sintofahamu kwani bado magari yanazuiliwa na kuendelea na safari hadi Kituo cha Kanisani na hivyo kusababisha usumbufu kwa Wananchi wa maeneo hayo. Kuna watu ambao hatujui ni Askari au Maafisa wa Manispaa, wanavaa sare za bluu, wanakaa karibu na round about wanazuia daladala zinazotaka kupeleka abiria au kwenda kuchukua abiria katika Kituo cha Buza Kanisani.
Tujajiuliza kwani ni hicho kituo kipya ni cha nani hasa mpaka Wananchi tunaendelea kuteseka hivi na wao hawajali? Kwani kuna kosa gani daladala zikija hadi Buza Kanisani? Au ndio wanalazimisha ili wanufaika wa Kituo kipya wapate fedha huku sisi tukiendelea kuteseka?
Pia soma:
~ Kituo kipya Buza kwa Mama Kibonge ni mradi wa nani? Mnatesa Wananchi kwa maslahi ya nani?
~ Maandamano ya Wananchi wa Buza - Dar es Salaam "Tumechoka tunamhitaji mkuu wa mkoa aje tunateseka"