Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Ukosefu wa uwazi, ugumu wa kupata taarifa sahihi kuhusu malipo, imekuwa changamoto kubwa kwa wanufaika wa TASAF.
Miradi ya TASAF kila sehemu inapaswa kuwafikia walengwa ambao ni Wazee na Wanawake wa Kaya masikini. Hali ni tofauti mkoani Kilimanjaro, katika Kata za Mnadani, Machame Narumu, Machame Mashariki na Machame Kaskazini, Wilayani Hai, ambapo kwa makusudi hakuna taarifa za idadi sahihi ya wanufaika wa TASAF.
Wapo wanufaika halisi, lakini pia wapo walioingizwa wasio na sifa ya kuwa wanufaika. Hata wanufaika hawafahamu haswa wanapaswa kupokea kiasi gani cha ruzuku kutoka TASAF.
Mnufaika kama Mwanamke (42), kutoka Kata ya Mnadani amekuwa akipokea malipo ya viwango tofauti tena baada ya Kufanya kazi za Mradi Kila siku za wiki, kiasi cha kushindwa kufahamu kiasi halisi anachopaswa kupokea. Mwaka 2023, malipo yake ya kwanza yalikuwa TZS 86,000/-, yakafuatiwa na TZS 54,000/- na kisha TZS 66,000. Malipo hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya miezi miwili. Wanufaika wengine katika Kata hiyo, Ni Mwanaume (63) na mkewe (53) ambao hupokea TZS 25,000 kila baada ya miezi miwili.
Fedha zinazotolewa na TASAF bado hazikidhi mahitaji muhimu ya familia na pia kumekuwa hakuna utaratibu mzuri wa malipo, kiasi kwamba wakati mwingine, wanufaika hupoteza fedha zao.
Wapo ambao hupita hata miezi minne kama ilivyo kwa Mnufaika Mwanaume (60), bila ya kuona malipo katika akaunti zao. Na hata pale wanapofuatilia katika ofisi za Kata, hujibiwa kuwa hilo lipo nje ya uwezo. Hata kwa wale wanaopata fedha zao kwa njia ya simu ya mkononi, wamekuwa wakikumbwa na kadhia ya kutokuona malipo, pindi fedha zinapotoka.
Ipo haja kwa Serikali kuangalia namna nyingine ya kuwasaidia walengwa, kwani njia inayotumika sasa haiwakomboi Wananchi kutoka katika umasikini. Njia ya sasa inazidi kuwadidimiza na kuwafanya kuendelea kuwa wategemezi kwa fedha ambayo haitoshelezi mahitaji muhimu na mara nyingi, haziwafikii walengwa.
Serikali iangalie namna ya kuwawekea miradi mbalimbali ya kiuchumi, hata kwa njia ya vikundi, kama vile ufugaji na kilimo cha kisasa, ambapo kwa kutumia miradi hiyo watakuwa wanajikomboa kiuchumi na kifikra.