Wanufaika wa TASAF (kaya masikini)waomba wafunguliwe miradi badala ya kupewa pesa mkononi maana hazijawahi kuwatoa kwenye umasikini

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Ukosefu wa uwazi, ugumu wa kupata taarifa sahihi kuhusu malipo, imekuwa changamoto kubwa kwa wanufaika wa TASAF.

Miradi ya TASAF kila sehemu inapaswa kuwafikia walengwa ambao ni Wazee na Wanawake wa Kaya masikini. Hali ni tofauti mkoani Kilimanjaro, katika Kata za Mnadani, Machame Narumu, Machame Mashariki na Machame Kaskazini, Wilayani Hai, ambapo kwa makusudi hakuna taarifa za idadi sahihi ya wanufaika wa TASAF.

Wapo wanufaika halisi, lakini pia wapo walioingizwa wasio na sifa ya kuwa wanufaika. Hata wanufaika hawafahamu haswa wanapaswa kupokea kiasi gani cha ruzuku kutoka TASAF.

Mnufaika kama Mwanamke (42), kutoka Kata ya Mnadani amekuwa akipokea malipo ya viwango tofauti tena baada ya Kufanya kazi za Mradi Kila siku za wiki, kiasi cha kushindwa kufahamu kiasi halisi anachopaswa kupokea. Mwaka 2023, malipo yake ya kwanza yalikuwa TZS 86,000/-, yakafuatiwa na TZS 54,000/- na kisha TZS 66,000. Malipo hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya miezi miwili. Wanufaika wengine katika Kata hiyo, Ni Mwanaume (63) na mkewe (53) ambao hupokea TZS 25,000 kila baada ya miezi miwili.
IMG-20240117-WA0022.jpg

Fedha zinazotolewa na TASAF bado hazikidhi mahitaji muhimu ya familia na pia kumekuwa hakuna utaratibu mzuri wa malipo, kiasi kwamba wakati mwingine, wanufaika hupoteza fedha zao.

Wapo ambao hupita hata miezi minne kama ilivyo kwa Mnufaika Mwanaume (60), bila ya kuona malipo katika akaunti zao. Na hata pale wanapofuatilia katika ofisi za Kata, hujibiwa kuwa hilo lipo nje ya uwezo. Hata kwa wale wanaopata fedha zao kwa njia ya simu ya mkononi, wamekuwa wakikumbwa na kadhia ya kutokuona malipo, pindi fedha zinapotoka.

Ipo haja kwa Serikali kuangalia namna nyingine ya kuwasaidia walengwa, kwani njia inayotumika sasa haiwakomboi Wananchi kutoka katika umasikini. Njia ya sasa inazidi kuwadidimiza na kuwafanya kuendelea kuwa wategemezi kwa fedha ambayo haitoshelezi mahitaji muhimu na mara nyingi, haziwafikii walengwa.

Serikali iangalie namna ya kuwawekea miradi mbalimbali ya kiuchumi, hata kwa njia ya vikundi, kama vile ufugaji na kilimo cha kisasa, ambapo kwa kutumia miradi hiyo watakuwa wanajikomboa kiuchumi na kifikra.

IMG-20240117-WA0026.jpg
 
ni wakati sasa kaya masikini kupewa mifugo na pembejeo za kilimo kama mbadala wa fedha
Kaya masikini nyingi zina mifugo, kwa mfano unaweza ona hio nyumba hapo ni poor lakini unakuta wanamiliki mbuzi kadhaa na kuku, ila pesa hawana, sasa ukiwapa mifugo watakuwa wanaiuza ili wale?
 
Ukosefu wa uwazi, ugumu wa kupata taarifa sahihi kuhusu malipo, imekuwa changamoto kubwa kwa wanufaika wa TASAF.

Miradi ya TASAF kila sehemu inapaswa kuwafikia walengwa ambao ni Wazee na Wanawake wa Kaya masikini. Hali ni tofauti mkoani Kilimanjaro, katika Kata za Mnadani, Machame Narumu, Machame Mashariki na Machame Kaskazini, Wilayani Hai, ambapo kwa makusudi hakuna taarifa za idadi sahihi ya wanufaika wa TASAF.

Wapo wanufaika halisi, lakini pia wapo walioingizwa wasio na sifa ya kuwa wanufaika. Hata wanufaika hawafahamu haswa wanapaswa kupokea kiasi gani cha ruzuku kutoka TASAF.

Mnufaika kama Mwanamke (42), kutoka Kata ya Mnadani amekuwa akipokea malipo ya viwango tofauti tena baada ya Kufanya kazi za Mradi Kila siku za wiki, kiasi cha kushindwa kufahamu kiasi halisi anachopaswa kupokea. Mwaka 2023, malipo yake ya kwanza yalikuwa TZS 86,000/-, yakafuatiwa na TZS 54,000/- na kisha TZS 66,000. Malipo hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya miezi miwili. Wanufaika wengine katika Kata hiyo, Ni Mwanaume (63) na mkewe (53) ambao hupokea TZS 25,000 kila baada ya miezi miwili.
View attachment 3007288

Fedha zinazotolewa na TASAF bado hazikidhi mahitaji muhimu ya familia na pia kumekuwa hakuna utaratibu mzuri wa malipo, kiasi kwamba wakati mwingine, wanufaika hupoteza fedha zao.

Wapo ambao hupita hata miezi minne kama ilivyo kwa Mnufaika Mwanaume (60), bila ya kuona malipo katika akaunti zao. Na hata pale wanapofuatilia katika ofisi za Kata, hujibiwa kuwa hilo lipo nje ya uwezo. Hata kwa wale wanaopata fedha zao kwa njia ya simu ya mkononi, wamekuwa wakikumbwa na kadhia ya kutokuona malipo, pindi fedha zinapotoka.

Ipo haja kwa Serikali kuangalia namna nyingine ya kuwasaidia walengwa, kwani njia inayotumika sasa haiwakomboi Wananchi kutoka katika umasikini. Njia ya sasa inazidi kuwadidimiza na kuwafanya kuendelea kuwa wategemezi kwa fedha ambayo haitoshelezi mahitaji muhimu na mara nyingi, haziwafikii walengwa.

Serikali iangalie namna ya kuwawekea miradi mbalimbali ya kiuchumi, hata kwa njia ya vikundi, kama vile ufugaji na kilimo cha kisasa, ambapo kwa kutumia miradi hiyo watakuwa wanajikomboa kiuchumi na kifikra.

View attachment 3007281
Hata hiyo miradi, ikishawapa hela, they will go back to square one. Ishu hapa ni matumizi bora na utunzaji wa fedha.
 
Ni maajabu sana ,uongozi wa nchi umeonelea kuwa ili kupunguza umasikini wa baadhi ya wananchi wake, njia sahihi ni kuwagawia hela cash 😆😆😆
 
Kaya masikini nyingi zina mifugo, kwa mfano unaweza ona hio nyumba hapo ni poor lakini unakuta wanamiliki mbuzi kadhaa na kuku, ila pesa hawana, sasa ukiwapa mifugo watakuwa wanaiuza ili wale?
Sasa kama baada ya miezi 2 mtu analipwa 50,000 au 60,000 je huwa wanakula nini hapo katikati?
 
Back
Top Bottom