Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kama unadhani maruhani yapo kwa viumbe hai utakuwa umekosea sana.. Maruhani yapo pia kwenye vitu visivyo na uhai na lugha pia
Hebu waza kwa makini usahihi wa sentensi kama hizi
1. Maji yameenda kuchotwa
2. Nimemkuta hayupo
Na watu daily wanazitumia bila shaka kabisa...
Sasa kuna hili la wanyama wanaotumika kama kiambishi cha ukwasi na starehe.. Nine's usiku mzima mfanano wake walau kwa mbali tu nimekosa kabisa
Nimechunguza kwa makini mno ni kwa namba yani vinashabihiana pia nimeshindwa kabisa
Mnyama kuku.. Kula kuku kwa mrija kama kiambishi cha ukwasi na mambo kuwa super.
Ni kawaida watu kuambiana ama kupiga umbea kwamba fulani sasa anakula kuku kwa mrija
Kuku si kimiminika... Kuku ni yabisi.. Mrija hutumika kunyonya ama kuupitisha vimimimika.. Mrija hauliwi ni nyenzo.. Kimimika hakitafunwi kinamezwa.. Sasa iweje mambo yakiwa safi tuambiwe tunakula kwa mrija? Walau basi wangesema tunafyonza kuku kwa mrija . Tena ni haya makuku mazezeta, nyama imelegea kama mlenda... Haya ni maruhani ya lugha
Mnyama bata.. Kufanya starehe na kiambishi cha kula bata! Mfanano uko wapi hapa sasa?
Pamoja na kwamba muimba taarab maarufu Marehemu Mzee Issa Matona aliwahi kuimba NYAMA ya bata ni tamu.. Naamini kwa dhati ya moyo alimaanisha kitu kingine kabisa. Kumbuka huyu ni Mzee wa Pwani ni mzaliwa wa mwambao..
Sasa inakuwaje kufanya starehe kitu ambacho ni cha furaha ama kupata nafuu fulani kulinganishwe na kula bata?kwani kufanya starehe ni uchafu?
Maana bata mwenyewe ni mmojawapo kati ya wanyama wachafu sana ndio maana Mondi kwenye moja ya tungo zake aliwahi kuimba.. Katoto (ka kike😀) kachafu kama bata...
Ukitaka kumfurahisha bata ajione yuko peponi muweke kwenye tope.. Utashuhudia anavyotikisa nyashi lake kwa furaha
Kula bata? Mpaka nyama ya bata ilete ladha inahitaji ufundi mkubwa sana.. Mapishi ya kuku si ya bata! Ukikosea kidogo tu nyama yake haliliki.. Kuna maji fulani machafu yaliyoko kwenye uti wake wa mgongo, utilises tu yakajichanganya na nyama hiyo mboga kaitupe tu maana haitalika
Mfanano uliopo ni mmoja tuu kwamba anayekula kuku kwa mrija mara nyingi ndiye anayekula bata.. Japo kinyume chake ni kwamba si kila anayekula bata basi anakula kuku kwa mrija!
Maruhani ya lugha haya
Good morning Tanganyika