Kumekuwa na madai yanayosambaa kuwa wanyama wa kufugwa kama paka na mbwa wanaweza kuwa na mzio (allergy) dhidi ya binadamu, hali inayodaiwa kusababishwa na mwili wa mnyama kuitikia kwa njia isiyo ya kawaida baadhi ya vitu vinavyopatikana kwa binadamu, kama vile chembechembe za ngozi, jasho au protini zinazotolewa na mwili.
Inadaiwa kuwa hali hiyo inaweza kumfanya mnyama kuonyesha dalili mbalimbali anapokuwa karibu na binadamu.
Inadaiwa kuwa hali hiyo inaweza kumfanya mnyama kuonyesha dalili mbalimbali anapokuwa karibu na binadamu.
- Tunachokijua
- Mfumo wa kinga wa wanyama wa nyumbani kama vile paka na mbwa hufanya kazi kama binadamu, ambapo unaweza kuzidisha mwitikio dhidi ya vitu visivyo na madhara na kusababisha mzio. Wanyama huathiriwa zaidi na aina kuu tatu za mzio: mzio wa chakula, mzio wa kuumwa na viroboto, au mzio wa mazingira kama vile vumbi, ukungu, na poleni.
Mzio huu husababisha dalili kuu mbili ambazo ni mwasho wa ngozi na matatizo ya mfumo wa kupumua. Katika baadhi ya matukio, paka wanaweza kupatwa na pumu inayochochewa na mzio, na matibabu yao kwa sasa yanajumuisha matumizi ya pampu za kupumulia (inhalers) zenye barakoa maalum zinazofanana na zile zinazotumiwa na watoto wa binadamu.
Madai
Je, wanyama wa kufugwa kama paka na mbwa wanaweza kuwa na mzio (allergy) dhidi ya binadamu?. (Dai hili linahusu kama seli za ngozi zilizokufa za binadamu au mba/dander zinaweza kuchochea mzio na pumu kwa wanyama wetu wa nyumbani).
Uhalisia
Madai haya ni Kweli, ingawa ni jambo linalotokea kwa uchache na nadra sana. Vyanzo vinathibitisha kuwa mba za binadamu zinaweza kuchukuliwa kama vitu hatari na mfumo wa kinga wa wanyama, hali inayoweza kuchochea mwasho wa ngozi pamoja na mashambulizi ya pumu kwa paka na mbwa. Hii inaonyesha kuwa changamoto ya mzio kati ya binadamu na wanyama hutokea pande zote mbili, ingawa wanyama kuathiriwa na binadamu ni nadra ikilinganishwa na visababishi vingine vya mzio.