Wanyama wanaoomba "Penzi"

Wanyama wanaoomba "Penzi"

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Huwa napenda sana kujua mahusiano ya kimapenzi kwa wanyama, nilichojifunza ni kuwa wanyama wengi wanapotaka kufanya mapenzi lazima dume amtoe mkuku jike na kumdhibiti ndipo anapopewa mchezo,mfano jogoo, beberu,paka n.k.
Lakini kwa upande wa njiwa dume ni tofauti, anachofanya ni kuomba na kubembeleza sana mpaka sometime anajigaraza hapo ndipo njiwa jike hupatwa na huruma na hulala chini huku akijibenua, na njiwa dume bila kufanya ajizi anapokea zawadi anayopewa. Kuhusu njiwa pia huwa habadilishi mpenzi kama wanyama wengine...sasa wana jf nanyi kama kuna wanyama mnaowajua tabia zao mnaweza kufafanua kidogo...
 
Kumbe memory yangu ime-expire! Nakumbuka kama beberu anaimbisha pia? Kuna kelele fulani anapiga wee hadi anapata vitu...
 
Duuu, hizi study inabidi ziende mbali zaidi... je kama hapa kweli twiga aliimbisha au alitumia ubabe???
 
Attachments

  • Twiga mchokozi.jpg
    Twiga mchokozi.jpg
    52.3 KB · Views: 219
Boflo,

Hizo ni reproductive strategies ambazo wanyama wanatumia kujionyesha how fit they are na jinsi gani wanaweza kuwa potential partners and fathers.
Ukisoma Animal behaviors utaelewa zaidi reasons behind all this.
Kifupi tu asilimia tisini ya ndege wote wanaomba "penzi" na ni monogomous wakati asilimia kumi tu ya mammals ni monogomous na majority wanatumia nguvu kumpanda majike...no time ya kumbembeleza🙂
 
wanyama na ndege wengi hubembeleza.

kitu kinachowafanya waonekane baadhi yao hawabembelezi ni lugha wanayotumia. mfano kuku utasikia wakitoa miguno fulanifulani kabla hajalikimbiza jike na kimrukia juu, na hata baada ya tendo hawagombani, utaona wakiendelea kufuatana kwani bado wanapendana, (siyo binadamu baadhi utawaona baada ya kulazimisha ama hata kubaka huwa kunajengeka uadui mkubwa badala ya mapenzi) pamoja na hayo huwa wanaomba mapenzi na hata kuku jike aombwapo mapenzi naye hujibu kwa kuguna pia na huwa wanaelewana miguno yao. msitake kufanya kila myama a-behave kama binadamu, Mungu aliumba kila kiumbe kwa namna yake. binafsi sijaona kiumbe akibaka zaidi ya baadhi ya wanadamu, viumbe wengine wote huwapanda majike baada ya kukubaliana ila lugha ndio tumeshindwa kuijua kwa hakika kuwa katika flirting zao huzungumza nini.

on top of that, hakuna kuimbe mwingine yoyote anayefanya mapenzi kimnyume cha maumbile wala anayefanya mapenzi bila lengo la kuzaa, ila binadamu tu! hili nalo ni la kujiuliza, kulikoni tukaw hivi wanadamu?

Glory to God
 
Buibui ndo kiboko. Dume anakaribia kiota cha jike ambaye anakuwa ametulia katikati. Dume akishajiridhisha kuwa jike yule ni strain sawa na yeye, hucheza tune fulani inayoendana na strain yake kwa kutumia nyuzi za kiota cha jike. ila mara kadhaa anakuwa amebugi na jike akisikia kuwa tune iliyochezwa sio ya aina yake huenda na kumuua hapo hapo jike. Ama kama dume alipatia, jike huenda na akampa yote.
 
Huwa napenda sana kujua mahusiano ya kimapenzi kwa wanyama, nilichojifunza ni kuwa wanyama wengi wanapotaka kufanya mapenzi lazima dume amtoe mkuku jike na kumdhibiti ndipo anapopewa mchezo,mfano jogoo, beberu,paka n.k.
Lakini kwa upande wa njiwa dume ni tofauti, anachofanya ni kuomba na kubembeleza sana mpaka sometime anajigaraza hapo ndipo njiwa jike hupatwa na huruma na hulala chini huku akijibenua, na njiwa dume bila kufanya ajizi anapokea zawadi anayopewa. Kuhusu njiwa pia huwa habadilishi mpenzi kama wanyama wengine...sasa wana jf nanyi kama kuna wanyama mnaowajua tabia zao mnaweza kufafanua kidogo...

nimependa sana style ya njiwa kama ni ya kweli, lakini unahitaji utafiti zaid wa tabia za wanyama
 
Back
Top Bottom