Wanyonge tuunganishe nguvu kumuokoa Diamond

FaizaFoxy Lady JD anapaishwa na muziki wakati Diamond anapaishwa na mashabiki ambao hawana misimamo na sio wa kudumu

Diamond atapaishwa bila kuwa mwanamuziki? ikiwa hivyo mbona hatumuoni ngafu kupaishwa? hata sijui ulichokiandika kina mantiki ipi!
 
Last edited by a moderator:
ewe punguani,kumbuka jide ni mtoto wa kike,ana kitu cha ziada ambacho daimond hana.au unataka awe bwabwa mwisho wa siku mumnyoshee vidole mtoto wa mwanamke mwenzenu?!.ebooo!,apambane kivyake.mbona prof jay kasimama japo hayuko kivile na team ruge.

Huo ubwabwa unapigiwa debe na Papa wa Vatikan kuhalalishwa, au umesahau?
 
Hivi Domo ana bifu na watu wa Ilala coz mara mbili alisema "watu wangu wa Kinondoni mpooooo, watu wangu wa Temeke mpooooo"
Ilala haikutajwa kabisa.
 
Siku ilikua mbaya sana jana kwa sisi mashabiki wa Dangote,

lakini naamini muda bado upo wakurekebisha alipo kosea
 
Kuna mtu anaweza kuodhesha dharau za diamond,maana mi nanona dharau dharau tu
 
Mie nadhani Diamond ajitathimini; Uhusiano wake na Mashabiki, hii Sio bure. Nakumbuka hata shoo moja mbeya ya kili tour Hakuwepo kwenye shoo lkn Walivyopiga nyimbo zake lol watu wanazomea vibaya mpk makopo yalihusika
 
Diamond ndiye nani tena mi namjua Ally Kiba alieimba Cinderella na Makmuga.
 
Diamond atapaishwa bila kuwa mwanamuziki? ikiwa hivyo mbona hatumuoni ngafu kupaishwa? hata sijui ulichokiandika kina mantiki ipi!

Utakapoacha kukurupuka kujibu ndipo utaiona hiyo mantiki vinginevo utakuwa unajibu kwa mhemuko siku zote
 
Last edited by a moderator:
Wangeweza wangemgaragaza Lady JD kwanza.

Namshauri Diamond aonane na Lady JD haraka iwezekanavyo apate maujanja.
Kwa mujibu wa imani yetu wewe unastahili kuchapwa bakora 57 kwa kusapoti mambo ya Haram. Ngoja nimuite sheikh.
 
HUU HAPA UTHIBITISHO.Mali ni nyingi nyumbani, kipi kimekukimbiza,Hapa Alikiba, anamwambia Diamond, nyumbani ( SHAROBARO RECORDS) kuna kila kitu, beats kali.....

Umetisha kijana!

Kumbe ndio maana halisi ya huo wimbo...daah, mie nilikua naserebuka na mamito kuwa wimbo mkali na mzuri kumbe ni marumbano ya hao madogo.

Kweli umri umenitupa mkono aisee....hahah!
 
Kafanyiwa nini?Au jf members wote walikwenda kwenye hyo fiesta?

Hili ndilo tatizo la Watanzania wengi. Ni kweli kuwa huyu kijana anajitahidi sana katika muziki wake na sio siri anakubalika na vijana walio wengi. Sasa hii haina maana kuwa na wengine wanaojibidisha kama yeye wasitambuliwe, kusifiwa au hata kulinganishwa nae.Mwanamziki kama Ali Kiba nae huwezi kumpuuza. Ni kijana mzuri tu kama Diamond na asingejisahau mno kwenye masuala ya muziki hata Diamond asindefua dafu kwake. Miziki na mashairi yake yametulia na yana mafunzo mengi huwezi kulinganisha na bata kavaa raizon.Ukiwashindanisha kwa kura toka kwa wapenzi wa mziki watachuana vikali na si ajabu Kiba kuibuka kidedea. Kazi ya muziki inahitaji mazoezi ya mara kwa mara kama walivyo wanasoka, wanariadha na inahitaji promotions na perfomances zq mara kwa mara. Wapenda muziki tungeshukuru kuwa nao hawa wasanii na tungewasifia na kuwaendeleza wote badala ya kufikiria kuwagawa.
 
kwanini msiunganishe hizo nguvu kuondoa umasikini wa watanzania wengi kuliko kuhangaika na mtu mmoja?? hio waachie wapambe wake wote.

Hoja kama hizi,mashabiki wake watakuona wewe wa ajabu au unawivu juu yake.msanii hajitambui mashabiki hawajitambui
.
 
Alivyokua anaimba jana alikua anazomewa vibaya sana.... watu wanamshabikia Ali kiba huku Diamond yuko stejini

Anasema watu wangu wa kinondoni vipi watu Booooo.. ndio hujuma inaongelewa hiyo..

Ndiyo kashapotea

Alianza kulalamika ujerumani akaenda uingereza na sasa tanzania......siku si nyingi atalalamikia mbagala
 
Utakapoacha kukurupuka kujibu ndipo utaiona hiyo mantiki vinginevo utakuwa unajibu kwa mhemuko siku zote

Huna jipya, naona unahororoja na kubwabwaja tu, nipishe mie.
 
Sasa ni wakati wa kukabidhi kijiti kwa wengne. Arudie ile kazi yake ya zamani kule mbagala na tandale mtogani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…