TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Kwa niaba ya sisi wanywa soda na vinywaji laini, naomba kufikisha malalamiko yetu kwa mheshimiwa mwenyekiti kuhusu vitendo visivyo vya staha ambavyo tumekua tukifanyiwa na jamii. Kati ya kadhia kubwa tunazokutana nazo ni hizi zifuatazo;
1. Kudharaulika na kuonekana hatuna hela/tumefulia. Hili halina ukweli wowote na tunalipinga kwa nguvu zote! Sisi wanywa soda ni wachangiaji wakubwa wa pato la taifa.
2. Kwenye vikao vya harusi na sisi tunalazimishwa kuchanga laki wakati soda ni Tsh 500 tu! Hivi kweli jamani hii inaingia akilini? Hasa ukizingatia soda huwezi kunywa zaidi ya mbili, nachangaje sawa na mtu anaefuta kreti ya bia?
3. Kuboeka kwenye shughuli. Tunapokua kwenye shughuli yenye pombe, sisi huanza kuboeka mapema maana hatuoni la maana. Sasa tukiaga kwamba tunataka kwenda nyumbani na saa hiyo ni saa mbili kasoro, mnaanza kutucheka.
4. Kutaniwa kwamba tunaleta nyuki. Ndugu zetu wanywa pombe kwa hili tunaomba mjiheshimu.
5. Kushindwa kwenda na kasi ya wanywa pombe. Haiwezekani kila raundi ya bia ikija na mimi mnaniletea soda. Matokeo yake unakuta nna soda 8 mezani na zote mnafungua, mi ntazinywa vipi? Acheni mambo ya kitoto.
6. Kuona mambo yote ya kijinga wanayofanya walevi. Sisi mda wote akili ziko sharp kwahiyo tunaona kila kitu jinsi wenzetu mnavyojiaibisha. Kesho yake tukija kuwaambia mnatuona wabaya.
7. Kuonekana sisi ni masnitch na hivyo kukwepwa na marafiki zetu walevi. Wewe ukilewa unaanza kushikashika wanawake na sisi tupo, unategemea nini?
8. Kulazimishwa kuendesha gari kuwasambaza walevi majumbani mwao. Watu wakishajua kwenye group yupo mnywa soda, utasikia "wewe leo utaturudisha nyumbani!" Hiyo kazi ya kuzunguka mji mzima kusambaza miili ya watu ambao hawajitambui imeshatuchosha
9. Kuulizwa ulizwa kwanini sisi hatujajenga hasa pale tunapowaambia ukweli ndugu zetu walevi kwamba bia moja ni sawa na tofali 2. Sasa hapo kuna uhusiano gani?
10. Kusingiziwa eti sisi ambao hatunywi pombe tunapenda wanawake! Hilo swala halina ukweli wowote jamani tunaomba mtuache.
Asanteni.