Wao wana pesa sisi Tuna Mungu

Wao wana pesa sisi Tuna Mungu

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2010 kama niko sahihi, Jimbo Arusha mjini lilikumbwa na kumezwa na usemi "Wao wanapesa sisi tuna Mungu". Usemi huu dhahiri ukaja kutumika kufanya kampeni ya kijana mmoja aliye na sura ya upole, mwenye mwonekano wa mapigano ya hoja ya kuweza kusemea na kuwakilisha Jimbo la Arusha mjini.

Chini ya picha katika bandiko hilo limeandikwa Chagua Godbless Jonathan Lema. Alionekana kama nabii aliyeshushwa na Mungu kuwapigania wananchi wasiojua kesho yao ila kwa kudra za Mwenye Enzi.

Upande wa pili wa nguzo kulikuwa na bandiko la kijani, lenye picha la mwanadada mrembo na mbichi kabisa limeandikwa, Chagua CCM chagua Ndg Batilda Buriani.

Nakumbuka wanajimbo wengi walisimama na chama tawala kipindi hicho, ila wakuwakilisha jimbo apewe kijana sasa. Na niliskia mzee mmoja toka kijiweni akisema tumpe huyu kijana sababu ni wa hali yetu. Wamama, vijana na wazee walisimama kwa kumuamini kijana.

Uchaguzi umetoka, matokeo hayatangazwi, vijana na wazee walienda andamana na kulinda mahesabu, kijana wao pendwa asiibiwe.

Niliskia kijana mmoja pembeni maisha yaliyomfanya asiogope chochote akisema, nitalinda kura yangu kwa jasho na damu.

Ushindi ukatangazwa, kijana jasiri na shujaa kashinda. Ilikuwa shangwe Jimboni, majumbani kwa kuamini Mungu kashusha nabii. Ukiangalia picha kwa nguzo za umeme, zinadhihirisha hakuna pesa.

Miaka ikasogea, kijana wetu kaingia maisha ya ukwasi akalevya akasahau hata wale waliolinda kura 2005, waliohatarisha maisha abaki na uongozi. Akapata fursa na kuondoka, kwenda kwa watawala babu zetu... kurudi vijana wakaenda mlaki aliechaguliwa mtetezi wao, waliambulia matusi, kebehi.. kuitwa wenye njaa... kuonesha mkombozi wenu ni mkwasi sasa, kapata anachotaka hana shida na nyie tena.. mnanuka umaskini, Ardhi maskini...

Na kusahau kauli kuwa

...wao (Ccm) wanapesa sisi Chadema tuna Mungu...

Maisha yanakwenda kasi sana....
 
Godbless Lema aliingia kwenye ubunge 2010, wewe ni muongo mfitini na wala sio mkazi au mpiga kura wa Jimbo la Arusha mjini.
 
Back
Top Bottom