TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Niseme tu mimi binafsi sina tatizo lolote na chanjo. Yaani kama ingekua sio huu uoga uliopitiliza wa sindano, mimi ningekua kati ya watu wa mwanzo kabisa kuchanjwa! Lakini mpaka leo bado nambwelambwela kwenda kuchanjwa kisa tu naogopa ile sindano. Kama mliona ile video ya mwanajeshi aliepelekwa kuchanjwa na kundi la wenzake kama 9 wamemshikilia na bado akawaponyoka na kukimbia, basi huyo ni mimi kabisaa..!!🤣
Sasa naomba kuuliza kwa wale ambao mmeshachanjwa hebu tupeni uzoefu hapa, je inauma? Au ni chwaaa... Imeisha iyo! Hapa nilipo sijawahi kuchoma chanjo yoyote pamoja na kuletewa chanjo izo bure kabisa kisa ni uoga.
Najua tupo wengi kwenye hili kundi japo mwenzetu mmoja ambae ni mkuu wa wilaya yeye tayari. Hebu tupeane akili hapa jinsi ya kuovercome huu uoga au mbinu gani tutumie?
Mwisho naiomba serikali iangalie uwezekano wa kutuletea chanjo za vidonge ione jinsi watu watakavyofurika kuchanja. Zikipatikana za kupaka pia itasaidia sana. Ieleweke uoga wa sindano ni "phobia" kama ilivyo uoga wa nyoka, tandu, vinyonga, nge, heights nk.