Waombaji wa ajira za kada za afya, majina yao yameorodheshwa

Waombaji wa ajira za kada za afya, majina yao yameorodheshwa

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Wizara ya Afya inapenda kuwataarifu waombaji wa ajira za kada za afya zilizotangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ajira.moh.go.tz tarehe 16 Aprili, 2022 hadi tarehe 03 Mei, 2022 kwamba zoezi la uchambuzi wa maombi ya kazi yaliyopokelewa limekamilika.

Waombaji waliokidhi vigezo ambao majina yao yameorodheshwa kwenye tangazo hili wanatakiwa kuzingatia yafuatayo;

Kuripoti katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mirembe – Dodoma ndani ya siku kumi na Nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

Kufika na cheti halisi na nakala mbili (2) kwa kila cheti ambacho kilitumika wakati wa kuomba ajira ikiwa ni pamoja na;


Nakala ya cheti cha kuzaliwa;

Wasifu binafsi (CV)

Nakala ya Kitambulisho/namba ya Uraia (NIDA);

Nakala ya vyeti vya elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne na Sita);

Nakala ya vyeti vya taaluma pamoja na Transcript;

Nakala ya Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship);

Nakala ya Cheti cha usajili kutoka Baraza na Bodi husika (Valid Licence);

Nakala ya Ithibati ya vyeti vya elimu na taaluma (Accreditation na Equivalence) kutoka TCU na NECTA kwa wale waliosoma vyuo nje ya nchi pamoja na wale waliosoma Sekondari nje ya nchi/Mitaala ya nje;

Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na Kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi;

Picha mbili (2) Passport Size.

Aidha, yeyote atakayeripoti na ‘Transcript’ tu au kuwa na nakala pungufu ya vielelezo tajwa hapo juu hatapokelewa.

Aidha, tunapenda kuwafahamisha kwamba, ajira hizi zimelenga kupunguza upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali, na kwamba uhitaji kuajiri wengine bado upo, hivyo waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili wafahamu kuwa hawakupata nafasi, hivyo wasisite kuomba tena wakati nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.

Waombaji wote mnasisitizwa kuzingatia muda wa kuripoti kazini kama ilivyoainishwa hapo juu. Wizara itachukua hatua ya kujaza nafasi hizo kwa wale ambao hawataripoti kwa siku zilizotajwa hapo juu.

Orodha ya waombaji waliopata ajira na vituo vyao vya kazi walivyopangiwa inapatikana kupitia tovuti ya Wizara ya Afya – www.moh.go.tz

Limetolewa na:-

Prof. Abel N. Makubi​


KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA

30 Juni, 2022

View attachment 2277867
 

Attachments

Afya hata kama wakikosa ajira kwa wao zipo nyingi hasa katika hospital binafis ni tofauti nawalimu na pia akili zao walimu ni manual ubongo wao wakufikiri huwa nimdogo sana
Nikweli jpo walimu kilio chao kinaisukuma serikali kuji tathmini upya ktk upande wa ajira
 
Juzi kwenye ajira za Tamisemi kuna nafas kama mia7 na point zilibaki bila watu na hiz za leo naona pia kuna nafas watu hawakupatikana so zitatangazwa tena...kweli Afya mpo vizuri
 
Juzi kwenye ajira za Tamisemi kuna nafas kama mia7 na point zilibaki bila watu na hiz za leo naona pia kuna nafas watu hawakupatikana so zitatangazwa tena...kweli Afya mpo vizuri
Hizo ambazo hazijazwa ni za madaktari bingwa..!!!

#YNWA
 
Back
Top Bottom