Wadau wa JF, naomba kuwaulizeni kuhusu waombaji wa vyuo vya afya kupitia tangazo la serikali la wizara ya afya na usitawi wa jamii. watu tulituma maombi siku nyingi lakini naona hakuna majibu. Kuna mtu kaniaambia kuwa majina hayo yametoka lakini nimetafuta kwenye website ya wizara ambayo ni www.moh.go.tz sijapata majina hayo. Naomba kama mdau, kama habari hizi na za kweli nisaidieni kujua wapi majina haya yanapatikana. make nimesubiri majina hayo wadau......