Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kilichojiri msibani ni pale waombolezaji walipomzomea Waziri wa Mambo ya Ndani mwenye dhamana ya Jeshi la Polisi Injinia Masauni. Ikumbukwe Injinia Masauni alipokuwa anajibu malalamiko ya wananchi kuhusu wimbi la polisi kuhusika na utekaji nyara na hata kuuawa kwa watu wakiwa mikononi mwa dola, alisema watu wanajiteka wenyewe na wanaendeza drama za utekaji nyara.
Hakustahuli kuwepo katika msiba kwa sababu inawezekana kabisa LABDA marehemu alijiteka nyara. Huyu waziri alistahili kuzomewa kwa sababu kwa nafasi yake alishatoa mwongozo unaolinda askari waendelee kuwadhuru watu.
Shime Watanzania. Tuchukue hatua sasa ya kuwazomea viongozi wote ambao kwa dhamana walizonazo wameshindwa kutuhakikishia usalama na uhai wetu.
Tuwapongeze sana waombolezaji wa mkoani Tanga kwa kuonesha nini tunapaswa kufanya
Hakuna aliye salama