Waombolezaji watoa Heshima za Mwisho wa Mwigizaji Grace Mapunda (Tessa) bila kufunguliwa Jeneza

Waombolezaji watoa Heshima za Mwisho wa Mwigizaji Grace Mapunda (Tessa) bila kufunguliwa Jeneza

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Mwili wa msanii, Grace Mapunda maarufu 'Tesa' umeagwa bila jeneza lake kufunuliwa.

Huo ulikuwa ni utaratibu wa familia ambao ulitangaza kutofunua jeneza lenye mwili wa muigizaji huyo. Taarifa hiyo imetolewa na mdogo wa marehemu, Moses Mapunda.

Baada ya taarifa hiyo, baadhi ya waombolezaji walianza kuondoka kabla ya kuanza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

hata utaratibu wa kufanya misiba ya halaiki kwenye viwanja vya mipira, karimjee, diamond jubilee, utaenda utakufa.
 
basi wabongo wataanza maneno maneno kama ilivyoada. Pumzika kwa amani mama Grace Mapunda
 
Ni hali ya kawaida kwa familia kutaka kulinda privacy ya ndugu yao.

Binafsi huwa sipendi kuangalia mwili wa aliyefariki unaweza ukajikuta unawaza ujinga bure kwa mawazo kama kwanini alikufa kafunga jicho moja au kwanini alikufa mdomo wazi huku mwenyewe sijui nitakufaje!
 
Wanaepusha maneno maneno yatakayowaumiza wanafamilia. Pia umati mwingi ule itachelewesha shughuli ya mazishi.
 
Utaratibu mzuri sana, nchi za nje nadhani mazishi huwa kunakuwa na privacy sana, sina hakika nadhani misiba mingine wanatoa na kadi ya mwaliko mkuu Kiranga unaweza kunipa elimu juu ya hili
 
hata utaratibu wa kufanya misiba ya halaiki kwenye viwanja vya mipira, karimjee, diamond jubilee, utaenda utakufa.
Sasa kaka msiba wako weŵ tukaweke karimjee kweli si matumiza mabaya ya fedha
 
Safi ni muhimu kulinda privacy ya marehemu na pia kuepusha hisia za dhambi zinazoweza kutoka kwa baadhi ya waombolezaji.

Tufike mahala tuone kifo ni kitu cha kawaida tu, na mtu akifika ikithibitika amekufa aandaliwe kwa taratibu zote na kuzikwa faster watu watawanyike wakafanye mambo mengine na kuiondolea mzigo familia ya marehemu.
 
Utaratibu mzuri sana, nchi za nje nadhani mazishi huwa kunakuwa na privacy sana, sina hakika nadhani misiba mingine wanatoa na kadi ya mwaliko mkuu Kiranga unaweza kunipa elimu juu ya hili
Msiba kama huo wa kadi nilishuhudia gangilonga iringa jiran alipofiwa
 
Safi kabisa, ulimbukeni wa kupitia kuangalia mfu hauna maana yoyote, halafu unakuta mtu anapita kuchungulia maiti anaanza kulia na kuanguka Tena ilihali marehemu si ndugu yake, ujinga mtupu.
 
Safi ni muhimu kulinda privacy ya marehemu na pia kuepusha hisia za dhambi zinazoweza kutoka kwa baadhi ya waombolezaji.

Tufike mahala tuone kifo ni kitu cha kawaida tu, na mtu akifika ikithibitika amekufa aandaliwe kwa taratibu zote na kuzikwa faster watu watawanyike wakafanye mambo mengine na kuiondolea mzigo familia ya marehemu.
Sielewi, mfano hisia gani?!!!
 
Sasa wanazunguka jeneza kufanya nini? Kama ni picha si ingewekwa tu mbele watu wakamuona bila kuzunguka
 
Safi sana!

Tunaanza kujielewa!
Nakerwa sana na misiba inayoaanika maiti!

Hakuna maiti nzuri! Iwe ya ajalia au kuugua!

Watu tuache upumbavu!
 
Back
Top Bottom