kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Wagonjwa wawili wameondolewa bughdha ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi maishani mwao baada ya kufanyiwa upasuaji na kupandikiziwa uboho wa binadamu au (Bone marrow), hatua inayosemekana kuondoa virusi vya HIV mwilini mwao.
Mgonjwa mmoja amesemekana kukaa kwa miezi minne bila ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi bila ya dalili ya kurejea kwa uogonjwa huo.
Madaktai waliofanya utafiti huo katika hospitali ya matibabu kwa wanawake ya Brigham nchini Marekani, wanasema ni mapema mno kuzungumzia uwezekano wa kutibu virusi hivyo kwani kuna unawezekano vinaweza kurejea wakati wowote.
Matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya Ukimwi.
Ni vigumu sana kutibu Ukimwi, kwa sababu hujifificha ndani ya DNA,ya mtu na hivyo kusababisha virusi sigu ambavyo haziwezi kutibika.
Madawa ya kupunguza makali ya virusi vya HIV hudhibiti virusi hivyo ndani ya damu lakini wakati mtu anapokosa kumeza dawa hizo, virusi hurejea.
Wanaume hao ambao hawajatajwa, wameishi na virusi hivyo kwa takriban miaka 30.
Wote walikuwa wanaugua aina ya saratani, aina ya lymphoma, ambayo ilihitaji wafanyiwe upasuaji.
Sehemu ya Uboho au Bone marrow ndipo celi mpya za damu hutengezwa mwilini na inaaminika kuwa ni kitovu cha virusi vya HIV mwilini.
Baada ya kufanyiwa upasuaji, hapakuwa na virusi mwilini kwa miaka miwili kwa mgonjwa mmoja wakati mwingine aliishi kwa miaka minne bila ya virusi kuonekana .
Ni mapema mno kuona kuwa upasuaji huo kama tiba ya ukiwmi na hata ikiwa itasemekana kuwa tiba basi sio tiba nzuri. Ni ghali mno na kwa baadhi ya wagonjwa kuna uwezekano wa kufariki ikiwa ni kwa asilimia15 hadi 20% kwa miaka ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji.
Wagonjwa hao sasa hawatumii tena dawa za kupunguza makali ya ukimwi. Upasuaji huu ulifanyiwa wagonjwa hao kwa sababu walaikuwa wanaugua saratani iliyohitaji matibabu.
Source: BBC