Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Muda mfupi baada ya kusitishwa kwa vita kunakotarajiwa kuendelea kwa siku 4 makundi ya wapalestina waliotiii amri ya kwenda kusini ya Gaza walionekana kuandamana kutaka kurudi makwao.
Jeshi la Israel lilisema watu hao hawatakiwi kuvuka barabara kuu ya Salahudin inayoigawa Gaza ya kusini na ya kaskazini.Mapambano yaliyotokea yalisababisha vifo vya raia watatu na wengine kujeruhiwa.
Muda mfupi baadae makundi ya raia walionekana wakizunguka huku na huko kwenye majumba yaliyobomolewa huku wakikushanya baadhi ya vitu vyao vilivyosambaratika.
Wapalestina hao wametamani bora wasingetekeleza amri hiyo ya kuingia kusini kwani huko nako wamekuwa wakipigwa na kuuliwa sambamba na msongamano mkubwa wa watu unaosababisha maradhi na shida mbali mbali za kimaisha.