Mi nashangaa sana wenye nyumba wetu wanadai kodi ya mwaka mzima kutoka kwa wapangaji wao wakati sisi ama watu wengi tunategemea/wanategemea mishahara ambayo tunalipwa kwa mwezi. Sasa hela ya mwaka mzima mimi ntaipata wapi? Let say mshara wangu kwa mwezi ni laki 3 (300,000/-) na kodi ya nyumba kwa mwezi ni sh 50,000/- kwa mwaka mzima inamaana sh 600,000/- na sasa nimlipe kwa mara moja. Je serikali haioni kuna umuhimu wa kubadilisha utaratibu huo? Je wanaJF mnaionaje hii imekaaje?