Wape watoto wako majina mawili ili wajue maana halisi ya uhuru

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Tunazaliwa, tunakuta baba anatuita fulani, mama naye.

Kaka pia anatuita hivyo, na dada na ndugu zetu! Kiukweli jamii nzima tumekuta inatuita tu fulanii fulanii.

Wapi tulikaa kikao, ni lini tulikubaliana kwamba jina langu, kitu muhimu ninachomiliki na kunitambulisha popote liwe ni hili na sio lile!?.

Na kizuri, au kibaya ni kwamba mda mwingine majina hayabaki kama majina tu. Kuna sifa na tabia zinazoambatana na jina husika. Tena mara nyingi ipo hiyo. Unabisha?

Quick fact check: Nikuulize, unamkumbuka yule mdada alikuwa anaitwa 1. Diana? Yule alokuwa anavaaga miwani, macho yalikuwa yanamsumbuaga hivii!!🤨. Kama umemsahau huyo je? Huyu wa pili, mtoto 2. Debora, toto toto kweli, yule binti alikuwa na macho fulani ivii yana mvuto yaani. Sijui ashaendaga wapi siku izi?😎

Umeona? Sasa kama majina yana uwezo wa kutuathiri kiasi hicho (kama umekubali lakini) kwa nini tusiwe makini wazazi;

Mosi: Kuwapatia watoto majina yanayoambatana na sifa nzuri, na matokeo mazuri maishani.
Pili: Kuwapatia majina mawili mawili yanayokuwa na matokeo (profile) tofauti tofauti ili zibalansiane.

Mfano 1. Unampa mtu majina mawili, moja la mchapa kazi masaa yote jingine la mla bata masaa yote. Ili aje abalansi, work and life balance.

Mfano 2. Unampa mtu majina mawili moja la kisasa ili aende na kila fasheni inayokuja, na la pili la kienyeji haswaa, gumu kwelikweli ili awe imara awe conservative. Yeye atabalansi kubadilika kupokea mazuri mapya ya kiteknolojia, na kun'gangana na mazuri ya asili ya kizamani..

Nahisi wasanii wameligundua hili jambo ndio maana wanajipa majina kadri ya sifa wanayoitaka kwa wakati huo. Anaweza kujiita chochote na akawa chochote. Akajiita simba, au Dangote anything tu na akawa. As a side note: unafikiri ni kwa nini wasanii wanaotumia majina yao halisi wana muelekeo wa kuwa authentic/halisi kuliko wanaojitungiatungia mfano Diamond VS Alikiba. Au akina Barnaba, Maua Sama?

Sasa unaonaje ukampa mtoto at least majina mawili ili akue akijua kabisa anao uhuru wa kuamua jamii imchukulieje yeye ajitambulishe yeye mwenyewe kwa utashi wake.

Na kama kichagizo (sijui kibwagizo? Mi sijui kiswahili chake)JE? Unajua username yako ulijitungia inabeba sifa na matokeo yepi (Profile)!?

Na ukiona jina ulilonalo linakuvutia nyuma, basi ni rahisi tu jipe AKA moja halafu jitambulishe! waambie watu wakuite hivyo na tayari unakuwa ushakuwa hivyo. Take control of your life. We make things happen💪. Eaaaaasy!
 
Wengine Bahati nzuri wazazi walishituka mapema walitupa majina mawili mawili sisi ndani mwetu kila mtu ana majina mawili la kisasa na la kibantu.
 
Huu upendeleo hata mimi nilipata na nimeona faida yake. Ni kitu nzuri for sure.
 
Umenikumbusha kuna mtoto mmoja wa kiume wa jirani yangu alikuwa anamajina mengi tangu nilipofahamu akiwa na miaka mitatu minne hivi. Alikuwa ana majina zaidi ya matatu anayoitwa hapo kwao
 
Tupe matokeo, je akili yake ilikuwaje alikuwa kichwa? Au jinga?

Alikuwa flexible? Au mgumu kubadilika?

Either way tabia alizokuwa nazo je? Sema hapo aidha ziwe nzuri au ziwe mbovu ni matokeo ya majina aliyoamua kuyakubali yawe yake kweli. Amefanya kwa utashi wake which is very powerful. Free-will. Hii ni nadharia tu lakini😎
 
Back
Top Bottom