Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wiki iliyopita nilipata ugeni wa ndugu yangu kutoka Pemba aliyeamua kutumia meli ya Azam inayotia nanga Tanga.Katika mazungumzo yetu alisema kila kitu katika safari kilikuwa shuwari lakini adha kubwa waliyoipata ni wakati wa kuteremka.Kwani lango kubwa la meli halikufunguliwa badala yake abiria wote na mizigo yao na watoto mgongoni walilazimishwa kupanda ngazi nyembamba ili wote haatimae wapite kwenye uchochoro mmoja wa meli kupata mlango kwenye mhudumu aliyekuwa na tochi ya kupima Ebola.
Kwa nje zoezi hili linaonekan lina nia njema ya kulinda afya za watanzania.Hata hivyo ukifikiri sana na kuonisha na mwahala mwengine duniani kwenye ukandamizaji kama ilivyo kule Palestina utagundua kuwa zoezi lote hilo lina mkono wa ukandamizaji kisiasa na kudhalilisha watu wa jamii fulani kuliko huko kulinda afya.
Pemba iko mbali sana baharini na mashariki ya kule kuliko na chimbuko la Ebola,Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.Hakuna lango lolote la kuingia Tanzania,mfano bandari au uwanja wa ndege wa kimataifa.Na wala hakujapatikana wagonjwa wenye maradhi hayo.
Hali hii inafanana sana na kule Palestina ambako mazlayuni wameweka vikwazo vingi vya kiusafiri kwa wapalestina.Kila wanakoelekea kuna mageti na kumtembelea ndugu aliye masafa yasiyofika nusu kilomita basi inaweza ikakuchukua siku nzima na gharama kubwa sana pamoja na kudhoofisha kiafya.
Wanaofanya hivyo si kwamba kuna faida yoyote halisi waipatayo bali ni furaha tu moyoni kuona binadamu mwenzake akidhalilika mbele yake.Maudhi hayo hawafanyiwi vijana tu wanaohofiwa kuwa wanaweza kuzua purukushani kwa hamaki za kuonewa,bali hufanyiwa wazee,watoto na wanawake na bila kuona vibaya.