Wapemba Ni watu poa sana

Nikweli mkuu,kuna mmoja alinisaidia sana kipindi cha nyuma,Anakukopesha hata mwaka mzima hana habari,hakuulizi,yeye anasema usipomlipa duniani,utamlipa akhera.

Ndio lugha zao hizo, mkuu ulishalipa?
 
Nimeishi na wapemba, Wapemba ndio wasomi wengi kati ya jamii ya makunduchi, Bwejuu, Mangapwani, Nungwi , Tunguu
Pia ndio wafanyabiashara hasa ila wale wengine ndio viongozi viongozi...
Ninao marafiki kadhaa kule wengi wakarimu na wacheshi
Yote tisa wapo wabaguzi hasa kule kwao, wanahisi wabara ni wahuni, malaya, makafiri n.k
 
Wapemba kwa mapishi No. 1 Chapati, Maandazi, Kalimati, kachori, Kababu, Sambusa, Vitumbua vya Maziwa, Mikate, Skonzi, Rost za maana, pilau, Biriani jamaa sembe kwao mwiko halipiti kooni

Tatizo lao ni Ubaguzi hasasasa wapemba ambao wamezaliwa na kukulia pembe ni wabinafsi na wabaguzi sana lakini hawa waliokulia Dar na Tanga hawanaga shida
 
Sawa ila ukitaka kujua ni wabaya kiasi gani ebu wadhulumu au mkorogane tuu akasirike ndo utaona ubaya wao
 
Unakuwa umelipiwa yahe"
 
Watu wengi wanashindwa kuwatofautisha wapemba na wazanzibari.
Ki ukweli kabisa wapemba ni watu smart sana hawanaga makuu na pia ni watu wa kazi haswaaa sio kama wazanzibari wazee wa urojo urojo.
Wapemba sio selfish na wachoyo kama wazenji, jamaa wana utu na upendo na ndio maana wanaweza kuishi sehemu yoyote na kukubalika, ila wazenji kutokana na tabia zao za hovyohovyo hawawezi kuishi popote zaidi ya zanzibar.
 
Nakumbuka kipindi nafanya saidia fundi kwa seremala mmoja hivi basi tukaenda kupiga kazi kwa mshua mmoja hivi kuna vifaa vilikua vinahitajika. Tukaandika bei za juu tukaenda kwa muuza duka tukamwambia tunakuja na bosi bei za kumtajia hizi hapa.

Akakubali.

Tukatoka na mshua hadi pale. Kufika tukapiga domo na bei zetu zile mshua akasema sawa. Mpemba akamwambia mshua "Hawa watu hawakufai, wameniachia hii karatasi ina bei wanazotaka nikutajie, tafuta fundi mwingine"

Mshua akamind akaondoka katuacha na tulitegemea gari lake nauli mifukoni hatuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…